Ni zamani lakini naikumbuka sana siku ambayo Mzee alitoa amri nisipewe chakula kwa sababu nilichelewa kurudi nyumbani.
Njaa iliniuma kwelikweli na jioni ile nikahisi itakuwa ndefu mno. Mara nikamsikia mama anasema "... wewee kamata hii ndoo kalete maji kisimani, ishike vizuri ndoo yangu..." Kwa unyonge nikaichukua ile ndoo, lkn nikahisi km kuna kitu ndani, sikuthubutu kuifungua. Nilipofika kisimani na kuifungua nikakuta mama kaniwekea bakuli la ubwabwa na nyama. Nililia kwa furaha, nikaupiga wote nikaosha chombo nikakiacha ndani ya ndoo niliyochotea maji. Niliporudi haraka haraka mama akaja kunipokea. Nikamwambie asante mama kwa sauti ya kunong'ona. Akajibu kwa sauti kali ambayo alihakikisha kila mtu anaisikia "...usirudie tena huo ujinga, hiyo ndio adhabu yako, leo utakoma nenda kalale...". *Aaah Mamaaaaa where are you my Queen? Mwenyezi Mungu awalinde wanawake wote*
Heshima kwenu wanawake wote duniani.
Heshima kwenu wanawake wote duniani.
…KAMA MAMA YAKO YUKO HAI COMMENT NAKUPENDA MAMA, KAMA KATANGULIA MBELE ZA HAKI COMMENT R. I. P MAMA …
@Aslay Isihaka
@Msanii bongofleva
@Aslay Isihaka
@Msanii bongofleva
No comments:
Post a Comment