Monday, 22 April 2019
Fahamu kuhusu Vita kuu ya Dunia
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilikuwa vita iliyopigwa
kuanzia mwaka 1914 hadi 1918 . Mataifa wapiganaji
yalikuwa Ujerumani, Austria-Hungaria , Bulgaria na
Uturuki (ziliitwa "Mataifa ya Kati", ing. central powers )
kwa upande mmoja dhidi ya Ufaransa , Urusi, Uingereza ,
Italia , Marekani na nchi mbalimbali zilizoshirikiana nazo
(zilitwa "Mataifa ya Ushirikiano", ing. allied powers ).
Vita hii ilianza katika Ulaya ikapanuka haraka hadi
Mashariki ya Kati , Afrika na Asia ya Mashariki
ikasababisha kifo cha takriban watu milioni tisa.
Sababu na matokeo
Sababu yake ilikuwa mashindano makali kati ya mataifa
ya Ulaya kuhusu kushika nafasi ya kipaumbele barani
Ulaya na duniani kote.
Matokeo yake yalikuwa mwisho wa kipaumbele cha
Ulaya duniani na kupanda ngazi kwa Marekani,
mapinduzi katika nchi mbalimbali, mwisho wa falme za
Ujerumani, Austria na Urusi pamoja na mwanzo wa
utawala wa kikomunisti katika Urusi, mwisho wa Dola la
Austria-Hungaria na wa Dola la Uturuki la Kiosmani
pamoja na mwisho wa ukoloni wa Kijerumani duniani.
Katika Ulaya nchi mpya zilijitokeza kama vile
Chekoslovakia , Ufini, Latvia , Estonia na Yugoslavia
pamoja na nchi za zamani zilizotokea tena katika
uwanja wa kimataifa ndizo Austria, Hungaria, Lithuania
na Poland.
Hali kabla ya vita
Sehemu kubwa ya Ulaya iliwahi kuwa na kipindi kirefu
cha amani tangu vita kati ya Ufaransa na Ujerumani
mnamo 1870- 1871 . Mataifa ya Ulaya yalikuwa na
mfumo wa mikataba na mapatano kati yao yaliyolenga
kuhakikisha uwiano wa mataifa. Mataifa makubwa ya
Ulaya yalikuwa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Urusi
na Italia.
Hali ilikuwa tofauti katika Kusini-Mashariki mwa bara
hilo. Hadi nusu ya pili ya karne ya 19 sehemu kubwa
ya Balkani ilitawaliwa na Milki ya Osmani iliyokuwa
milki ya Kiislamu ya kutawala Wakristo wengi. Milki hii
iliendelea kudhoofika wakati wa karne ya 19. Nchi
mbalimbali zilijitenga na kupata uhuru, kama vile Ugiriki,
Serbia , Bulgaria na Romania . Nchi hizi mpya zilipigana
kivita kati yao na Milki ya Osmani hadi mwaka 1912.
Mwanzo wa vita
Vita Kuu ilianza kutokana na ugomvi kati ya Austria-
Hungaria na Serbia. Kutokana na muundo wa mikataba
ya kusaidiana kati ya nchi za Ulaya mwanzo huo
ulisababisha mfululizo wa hali ya vita kati ya mataifa,
na mengine ya Balkani yalitafuta uhuru wao.
Tarehe 28 Juni1914 katika mji wa Sarayevo, Bosnia ,
mwana wa Kaisari wa Austria aliyekuwa mfalme mteule
aliuawa pamoja na mke wake na mgaidiMserbia
mwanachama wa kundi la " Mkono Mweusi " lililopinga
utawala wa Austria-Hungaria katika Bosnia . Austria
iliamuru Serbia ifuate masharti makali katika uchunguzi
wa tendo lile. Serbia ilipokataa sehemu ya mwisho ya
masharti, Austria ilitangaza hali ya vita dhidi ya Serbia
tarehe 28 Julai1914 .
Agosti ya 1914 iliona kupanuka kwa vita hii: Warusi
walikuwa na mkataba wa usaidizi na Serbia
wakatangaza hali ya vita dhidi ya Austria-Hungaria.
Hapo wakaingia Wajerumani waliokuwa na mapatano
ya usaidizi na Austria-Hungaria wakitangaza hali ya vita
dhidi ya Urusi. Urusi kwa upande wake ulikuwa na
mkataba wa kusaidiana na Ufaransa, kwa hivyo hali ya
vita ikajitokeza pia kati ya Ufaransa na Ujerumani.
Uingereza ulijiunga na vita baada ya Wajerumani
kuanza kuingia eneo la Ubelgiji kwa shabaha ya kuvuka
haraka ili wavamie Ufaransa Kaskazini.
Kuanzia Oktoba 1914 Milki ya Osmani ( Uturuki) ilijiunga
na vita kufuatana na mkataba wake wa siri na
Ujerumani.
Mwaka 1915 Italia ilijiunga na Wafaransa na
Waingereza kwa kushambulia Austria-Hungaria, ingawa
awali ilikuwa na mkataba na dola hilo.
Vita katika nchi mbalimbali
Vita ilipigwa kwa ukali miaka ya 1914-1918.
Wajerumani waliingia ndani ya Ufaransa lakini
walikwama kabla ya kufikia jiji kuu la Paris. Kwa muda
mrefu mstari wa mapambano ulibaki palepale.
Katika Mashariki Wajerumani walifaulu kurudisha
mashambulio ya Kirusi na kuteka sehemu za Urusi.
Katika Kusini mwa Ulaya Waustria walifaulu kwa shida
kubwa kuteka Serbia na Montenegro pamoja na
Albania.
Waturuki walishindwa kwa ujumla katika mashambulio
yao dhidi ya Warusi katika eneo la Kaukazi na dhidi ya
Waingereza katika Misri . Lakini walifaulu kuzuia
Waingereza wasifike Uturuki penyewe. Waingereza
walipeleka jeshi katika Irak ya kusini wakafaulu
kuwarudisha Waturuki hadi kaskazini ya nchi hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment