Tuesday, 5 March 2019

Njia ya uzazi wa mpango ya Vipandikizi-6


Kipandikizi ni kifaa kidogo cha plastiki mfano wa njiti za kiberiti, ambacho huwekwa chini ya ngozi sehemu ya juu ya mkono na mtoa huduma mwenye ujuzi. Hii ni njia ya uhakika na ya muda mrefu. Wanawake 99 kati ya 100 wanaotumia vipandikizi hawawezi kupata ujauzito.


Hutoa kichocheocha aina ya projestini ambacho hufanana na kichocheo cha asili cha mwili wa mwanamke. Mwanamke anaweza kupata ujauzito mara tu anapotoa vipandikizi.
Hapa Tanzania kuna aina mbili za vipandikizi:
• Kipandikizi aina ya implanon: hiki ni kipandikizi chenye kijiti kimoja ambacho kinafanya kazi kwa miaka mitatu
• Kipandikizi aina ya Jadelle: hiki ni kipandikizi chenye vijiti viwili ambavyo vinafanya kazi kwa miaka mitano
Jinsi zinavyofanya kazi
Vipandikizi vinasababisha ute mzito kwenye shingo ya kizazi na kuzuia mbegu za kiume zisikutane na kurutubisha yai. Pia inazuia yai kupevuka
Faida
• Ina ufanisi mkubwa na salama
• Inayo kinga ya miaka mingi ya kuzuia ujauzito
• Mtumiaji haihitaji kufanya chochote baada ya kuekewa
• Ni nzuri na yenye usiri
• Haingiliani na kujamiiana
• Inaweza kutumiwa na mwanamke anayenyonyesha wiki sita baada ya kujifungua
• Inasaidia kuzuia magonjwa ya nyonga na upungufu wa damu wa aina ya madini chuma
• Inapunguza matatizo ya utungaji mimba nje ya kizazi
• Inafaa kutumiwa na wanawake wote pamoja na akina mama wenye maambukizi ya VVU.
Maudhi madogo madogo yanayoweza kujitokeza
Baadhi ya wanawake hupata maudhi madogo kama yafuatayo
• Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi kama: mfano matone matone ya damu au kutopata hadhi kabisa.
• Maumivu ya kichwa, maumivu ya tumbo, kutokwa na chunusi, kuongezeka uzito wa mwili, maumivu ya matiti, kizunguzungu, mabadiliko ya hisia na kichefu chefu
Ni nani anaweza kutumia vipandikizi
Vipandikizi ni njia salama na inayofaa kutumiwa karibia na wanawake wote.
Mwanamke asitumie kipandikizi endapo:
• Ananyonyesha mtoto mwenye umri chini ya wiki sita
• Matatizo makubwa ya ugonjwa wa ini au saratani ya ini
• Mwanamke anayetokwa na damu ukeni isiyo ya kawaida na ambaye tatizo lake
halijabainishwa kitaalam
• Ana au aliwahi kuwa na saratani ya matiti

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!