Sunday, 3 March 2019
JINSI KIFUNGUA KINYWA BORA'BREAKFAST' KINAVYO IMARISHA AFYA:
Unapolala mwili huwa upo kazini kumen'genya vyakula tulivyokula na vinywaji tulivyokunywa kabla ya kulala,tunapoamka,mwili uko tayari kupata kifungua kinywa baada ya kukaa kwa muda mrefu bila chakula.
Kiwango cha sukari katika damu huwa imepungua mtu anapoamka kwa kuwa alikuwa hali wakati wa kulala,sukari iliyomo katika damu huingizwa katika seli na kuunguzwa na hivyo kuipa misuli na ubongo nishati. Kupata kifungua kinywa kwa wakati ni kuupa uhai mwili na akili,kukosa mlo wa asubuhi sio tu mwili unakuwa dhaifu bali pia ni hatari ya kupata magonjwa kama vile kisukari,kiharusi,unene na uzito kupita kiasi na magonjwa ya moyo pia mtu akikosa mlo wa asubuhi njaa huwa kubwa na hivyo humsukuma mtu huyo kula kila aina ya chakula pale atakapoamua kula na pia atakula kupita kiasi hali inayochochea magonjwa tajwa hapo juu.Kwahiyo ni vema kupata kifungua kinywa japo kiasi kidogo kabla ya saa moja kupta baada ya kuamka ni jambo muhimu sana kwa afya ya mtu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment