Thursday, 22 November 2018

ATUHUMIWA KUMUUA NA KUMFANYA KITOWEO MPENZI WAKE

Image may contain: food
Mwanamke mmoja raia wa Morocco anatuhumiwa kumuua mpenzi wake na kumfanya kitoweo huko Falme za Kiarabu, waendesha mashtaka wanasema.

Tukio hilo linadaiwa kufanyika miezi mitatu iliyopita, laikini limegundulika hivi karibun baada ya jino la binaadamu kuonekana kwenye mashne ya kusagia matunda ya mwanamke huyo.

Mtuhumiwa huyo amekiri kutenda makosa hayo, na kuseam ulikuwa wakati wa "uwendawazimu", gazeti la serikali la The National linaripoti.

Mwanamke huyo ambaye yupo kwenye miaka ya 30 atapandishwa kizimbani baada ya kukamilika kwa uchuguzi.

Wapenzi hao walikuwa katika mahusiano kwa miaka saba. Kwa mujibu wa The National, mwanamke huyo alimuua mpenziwe baada ya kumwambia kuwa alikuwa anapanga kumuoa mwanamke mwengine kutoka Morocco.

Japo polisi hawajaeleza ni namna gani mauaji hayo yalitekelezwa, wamesema alikata mabaki yake na kupikia chakula cha asili cha wali na nyama na kuwapa wafanyakazi raia wa Pakistani.

Tukio hilo iligunduliwa mara baada ya kaka wa marehemu kwenda kumsaka katika nyumba aliyokuwa akiishi na mwanamke huyo katika mji wa Al Ain, ulio mpakani na nchi ya Oman. Wakati akiendelea na msako akaliona jino la mwanadamu kwenye mashine ya kusaga matunda.

Kaka huyo ikabidi kwenda kuripoti polisi, na mara baada ya kufanyika vipimo vya kinasaba vya DNA iligundulika kuwa ni jino la ndugu yake.

Kwa mujibu wa polisi, mwananmke huyo kwanza alimwambia ndugu wa mpenziwake kuwa waligombana na marehemu na alimfukuza nyumbani kwao. Baadae inadaiwa alizimia alipokuwa anahojiwa na polisi na baada ya kuzinduka alikiri kutekeleza mauaji hayo.

Imeripotiwa kuwa aliitisha usaidizi wa rafiki yake ambaye bado hajatajwa kusafisha nyumba baada ya mauaji.

Mtuhumiwa huyo kwa sasa yupo hospitalini ambapo anafanyiwa uchunguzi wa kiakili.

Source: BBC Swahili

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!