Thursday, 4 October 2018

Fanya hivi ili mtoto asipate Matege

Vitamin D ni mojawapo ya Virutubisho muhimu ambavyo mwili unaweza kutengeneza kwa msaada wa mwanga wa jua. Kumuweka mtoto kwenye jua kwa muda wa nusu mara moja kwa wiki inatosha kutengeneza vitamin D ya kutosha kutumiwa na mwili kwa muda wa wiki moja.


Hata hivyo haishauriwi kuwaweka watoto wadogo wenye umri wa chini ya miezi sita kwenye jua kwa sababu inaongeza hatari ya kupata kansa ya ngozi wanapokuwa wakubwa.
Faida za vitamin D
Vitamin D husaidia mifupa kuwa imara, husaidia kinga ya mwili kuimarika hivyo kumsaidia mtoto kupambana na maradhi. Pia vitamin hupunguza hatari ya mtoto kupata Ugonjwa wa kisukari anapokuwa mtu mzima.
Upungufu wa vitamin D husababisha nini?
Upungufu wa vitamin D husababisha ugonjwa wa Matege(rickets). Watoto wenye umri wa kati ya miezi 3 hadi 18 wako katika hatari kubwa ya kupata maradhi haya. Matege husababisha mifupa kuwa dhaifu, hivyo kupinda na kuuma.
Upungufu wa vitamin D pia huongeza hatari ya mifupa kuvunjika miongoni mwa watoto wakubwa, vijana na watu wazima. Licha ya kwamba upungufu hutokea mara nyingi katika maeneo ambayo hayapati mwanga wa jua wa kutosha lakini hata kwenye maeneo yetu yenye jua la kutosha watoto hupata upungufu wa Vitamin D.
Vyanzo vya vitamin D
Chanzo kikuu cha vitamin D ni mwanga wa jua. Vyanzo vingine ni vyakula aina ya samaki na mayai, maziwa ya ng'ombe pamoja na vyakula vilivyoongezewa vitamin D. Maziwa ya mama hayana kiwango cha kutosha cha vitamin D. Maziwa ya kopo(infant formula) yana kiwango cha kutosha cha vitamin D.
Ufanyaje ili mwanao apate Vit D ya kutosha
Iwapo mama anayenyonyesha hatumii vidonge vya kuongeza Vitamini inapendekezwa kuwa mtoto mchanga apewe matone ya vitamin D wiki chache baada ya kuzaliwa mpaka mtoto atakopachishwa na anatumia vyakula vilivyoongezwa Vit D au maziwa ya ng'ombe. Pia mama anayenyonyesha anaweza kutumia vidonge au vyakula vyenye Vitamini D
Chama cha Madaktari wa Watoto cha nchini Marekani hatupendekezi matumizi ya Mafuta ya samaki (fish oil) na cod liver oil kama vyanzo vya vitamin D miongoni mwa watoto.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!