
Mwanadiplomasia huyo mashuhuri amefariki asubuhi ya leo huko nchini Uswisi baada ya kuugua kwa muda mfupi
Kutokana na umahiri wake Kofi Annan alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Desemba 1996. Na alianza kazi rasmi Januari 1, 1997
Mwaka 2001 alichaguliwa kwa mara ya pili kuuongoza tena Umoja wa Mataifa. Oktoba 12, 2001 alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel
Annan alianza kutumikia nafasi mbalimbali ndani ya Umoja wa Mataifa(UN) tangu mwaka 1974 ingawa aliacha kazi na kurudi kuiongoza Kampuni ya Utalii nchini kwake (GHANA)
Mwaka 1976 alirudi tena kwenye ulingo wa siasa za kimataifa na safari yake ndani ya Umoja wa Mataifa ikaanza rasmi.
Kofi Atta Annan alizaliwa mnamo Aprili 8, 1938













No comments:
Post a Comment