Wednesday, 22 August 2018

Mambo ya kufahamu kuhusu mtoto kuanza kuota meno


Je wakati gani meno huanza kuota?
Uoataji wa meno hutofautiana kati ya mtoto wa kiume na wa kike. Mtoto wa kike anawahi kuota meno kuliko yule wa kiume. Kwa wastani watoto wengi huanza kuota meno wanapokuwa na umri wa miezi sita.
Je meno yapi huanza kuota



Kwa kawaida meno mawili ya chini huanza(meno ya mbele). Kisha hufuatia meno manne ya juu. Baada ya hapo meno mengine huendelea kuota mara nyingi huota mawili mawili(moja moja kila upande).
Je mtoto mdogo ana meno mangapi?
Binadamu ana meno ya aina mbili. Meno ya utoto na meno ya kudumu. Hivyo mtoto mdogo ana meno ya utoto 20. Kila taya inakuwa na meno kumi. Meno ya utoto yanaanza kung'oka mtoto anapofikisha umri wa miaka sita.
Je kwanini ni muhimu kutunza meno ya mtoto
Licha ya kwamba meno ya utotoni hung'oka lakini kuhakikisha meno ya mtoto yana lindwa na kutunzwa vizuri kwa sababu zifuatazo:-
Meno ya utotoni husaidia mtoto kutamka baadhi ya maneno vizuri
Meno ya utotoni hutengeneza njia ya meno ya kudumu
Meno ya utotoni husaidia sura na umbo la uso kukuwa vizuri
Husaidia mtoto kuwa na afya njema kwa sababu hutafuna chakula.
Je dalili zipi huashiria mtoto kuanza kuota meno?
Watoto wengi wanao ota meno huonyesha dalili mbalimbali mfano kusikia maumivu mdomoni, kuwashwa pamoja na kutoka mate kwa wingi.
Je jamii inaamani nini?
Watu wengi wakiwemo wataalam wa afya huamini kuwa homa pamoja na kuharisha ni dalili za kuota meno. Hata hivyo tafiti mbalimbali zimetahadharisha kuwa imani hiyo inaweza kuatarisha afya ya mtoto na dalili hizo sio dalili za mtoto kuanza kuota meno
Kuchelewa kuota meno
Wakati mwingine mtoto anaweza kuchelewa kuota meno. Iwapo hali hiyo imetokea muone Daktari wa meno atakushauri zaidi.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!