Kenya, Ruth Kamande ni binti aliyewahi kushinda taji la U-miss Lang’ata Prison 2016 ambaye mapema jana amehukumiwa kifo mara baada ya kukutwa na hatia ya kuua kwa kutaka akiwa na umri wa miaka 21.
Mnamo 2015 binti huyo aliingia katika mgogoro mzito wa kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wake, Farid Mohamed na kujichukulia uamuzi wa kumuua kwa kumchoma mpenzi wake visu 22.
Ndugu wa marehemu Farid Mohamed wamefurahishwa na hukumu iliyotolewa na mahakama ya kumuhukumu kifo mlimbwende huyo kwani wameona mahakama imetenda haki.
No comments:
Post a Comment