Timu ya taifa ya Senegal leo imeshuka uwanjani kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya timu ya taifa ya Poland, Senegal imeanza vizuri dhidi ya timu zote za taifa za Afrika zilizocheza Kombe la Dunia 2018.
Bara la Afrika lina timu tano pekee zinazoshiriki michuano ya Kombe la dunia lakini hadi Senegal anacheza na Poland kulikuwa hakuna timu ya Afrika iliyokuwa imefanikiwa kupata point hata moja zaidi ya Senegal leo kufungua milango kwa kuifunga Poland kwa magoli 2-1.
Magoli ya Senegal yalifungwa na Cionek aliyejifunga dakika ya 38 na M’baye Niangaliyefunga goli la pili dakika ya 61, wakati goli pekee la Poland lilifungwa na Krychowiakdakika ya 86, ushindi huo sasa unawaweka pazuri Senegal na wanatakiwa kushinda mchezo ujao ili kusonga mbele.
No comments:
Post a Comment