Saturday 17 March 2018

KUNGUNI MBEYA: “Ni marufuku kuendelea, kila mtu apambane na hali yake.”-Makalla


Wananchi wa Kata ya Igurusi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, wamechangishana fedha kwa ajili ya kumlipa mganga wa kienyeji ambaye walimuita ili awasaidie kuondoa kunguni katika makazi yao.

Mbali na kunguni, wananchi hao wamedai kuathiriwa na viroboto na chawa kwenye makazi yao wakiamini wadudu hao wamepelekwa kishirikina. Zoezi hilo hata hivyo limewagawa wananchi hao katika makundi mawili, baadhi wakiunga mkono na wengine kupinga.
Mgongano huo umesababisha kuwapo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani katika kata hiyo, kumfanya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, kuingilia kati na kupiga marufuku zoezi hilo huku akisema hata kwa bahati mbaya hawezi kuruhusu watu kuamini uchawi katika mkoa wake.
“Mimi sasa hivi naelekea Dodoma kikazi, sasa nikiruhusu zoezi hilo ambalo ni kinyume na sheria za nchi sitafika hata Iringa, nitakuwa nimeshatumbuliwa na rais,”-Makalla.
“Ni marufuku kuendelea… kila mtu apambane na hali yake.”-Makalla

Crd: MillardAyo.com

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!