Saturday, 24 February 2018

Simulizi zenye mafunzo za Jakaya Kikwete

Related image
RAIS wa zamani wa Tanzania, Dr. Mrisho Jakaya kikwete, alipata KUSIMULIA:
"Siku moja usiku, nilipokuwa mtoto, nakumbuka kumwona MAMA yangu akituletea chakula mezani nikiwa na BABA.
MAMA aliniwekea sahani ya CHAPATI, huku akimwekea BABA sahani yenye chapati ILIYOUNGUA.


Nilijaribu kumuangalia BABA ili kuona ATAFANYAJE. Baba alianza kula CHAPATI ile iliyoungua huku akiniuliza kuhusu maendeleo yangu shuleni.
Sikumbuki nilichomjibu, ninachokumbuka ni kumsikia MAMA akimtaka RADHI baba kwa KUUNGUZA chapati. Na kamwe sitasahau majibu ya BABA pale alipomjibu MAMA kwa kumwambia, 'Oh, usijali MKE WANGU. Huwa NAPENDA pia chapati za KUUNGUA.'
Baadaye , nilipokwenda kwa baba na kumtakia usiku mwema, ndipo nilipomuuliza kama ni kweli hupendelea chapati za kuungua.
Alianza kuniambia, 'Leo, MAMA yako alitingwa mno na MAJUKUMU ya kazini hata akawa amechoka sana, ndipo akaunguza chapati. Lakini, kwa bahati, chapati ILIYOUNGUA haiwezi KUMUUMIZA mtu kiasi cha KUMCHOMA MOYONI, walakini MANENO makali yanaweza KUMUUMIZA. Hivyo, sikuwa na sababu ya KUMSHUTUMU kwa MANENO makali. Hata kama sipendi chapati za kuungua, ila kumjibu vile kumemfanya awe huru. Unajua MAISHA nayo hayako KAMILI kama TUSIVYO kamili SISI wanaadamu. Kwahivyo, ili kudumisha FURAHA na kuboresha MAHUSIANO na MAELEWANO baina YETU, ni lazima TUJIFUNZE kuyakubali na kuyakabili MAPUNGUFU yetu - Chapati za kuungua hazidumu milele, zikishasagika tumboni utakwenda kuzitoa msalani. Lakini, MANENO makali huacha majeraha ya kudumu MOYONI

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!