Thursday, 15 February 2018

Polisi kuchunguza kifo chenye utata Coco Beach

Image result for coco beach dar es salaam
JESHI la Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam, limesema linachunguza ili kubaini chanzo cha kifo cha mtu ambaye mwili wake uliookotwa katika ufukwe za Coco eneo la Masaki jijini Dar es Salaam.


Hata hivyo, limesema haliburuzwi na kauli za hisia, zinazotolewa na baadhi ya watu na hata wanasiasa kuhusisha kifo hicho na watu wanaodaiwa kujifanya kuwa askari wa Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Jumanne Muliro alisema jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa msamaria mwema Jumatatu asubuhi kuwa katika ufukwe huo, kuna mwili umeonekana, ambao unakadiriwa kuwa wa umri wa miaka 30 hadi 35, ukidaiwa kuwa na majeraha.
Alisema polisi walikwenda katika ufukwe huo na kukuta mwili huo, ukiwa na majeraha mikononi na kichwani. Mwili huo ulipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kubainika kuwa mtu huyo amekufa.
Kamanda Muliro alisema jeshi hilo, linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
Kuhusu kuhusisha mwili huo na mwanachama wa Chadema, Kamanda huyo alisema jeshi hilo halifanyi kazi kwa hisia za mtu, na wala hawaburuzwi na liachwe lifanye uchunguzi kwa mujibu wa taratibu zao.
Kamanda Muliro alisema hali ya usalama katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam ni salama kwa ujumla kutokana na ripoti kuonesha hivyo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!