Tuesday, 13 February 2018
MOROGORO: Kilo zaidi ya 21 za nyama ya Mbuzi na Ng’ombe zisizo na ubora zimekamatwa na zimeteketezwa kwa moto.
Timu ya watalaamu wa mifugo kutoka Bodi ya nyama Tanzania wamefanya operesheni ya kustukiza katika mabucha yanayouza nyama na mabaa yenye majiko yakuchoma nyama na kubaini baadhi ya nyama zinazouzwa hazina ubora na zinaweza kusababisha maambukizi yamagonjwa mbalimbali yatokanayo na mifugo ikiwemo kifua kikuu na homa ya vipindi ambapo zaidi ya kilo 21 za nyama ya mbuzi zimekamatwa na kuteketezwa kwa moto.
Kufuatia wafanyabiashara hao kukutwa wakiwa hawajakizi vigezo pamoja na mambo mengine ikamlazimu afisa nyama bodi ya nyama Tanzania Edgar Mamboi kutoa elimu kwa wauzaji wa nyama ili wakidhi vigezo.
Mohamed Chamzhim ni Afsa mifugo na uvuvi Manispaa ya Morogoro ambapo amewataka wakazi wa Manispaa hiyo kuwa makini na nyama hizo wakati zoezi hilo la operesheni likiendelea.
ITV
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment