Friday, 9 February 2018

`Matumizi mabaya ya simu, chanzo kikubwa cha vurugu ndani ya ndoa`!

 Mfano wa bibie aliyempigia shugadadi wake lakini bahati mbaya simu haikupokelewa. Huku nyumba mkewe akaifuma simu ile na alipopiga namba ile, bibie akaitikia …halo baby…halooo baby…lakini mke wa jamaa akauchuna kimya simu ikakatwa. 
 
Ndipo bibie akatuma ujumbe mfupi wa simu…’baby mbona unapiga nikipokea unakaa kimya?(bila kujua kumbe aliyekuwa na simu ile ni mke wa jamaa). Kilichofuata pale ni mtafaruku ndani ya ndoa ile haijulikani iliishaje!  

Simu zimekuwa kichocheo kikubwa katika kuzipa misukosuko ndoa nyingi na  hela nazo zinamsumbua, dharau zinakuwa nyingi kwenye ndoa”.
 
Mpenzi msomaji, hebu sasa fuatilia maoni ya baadhi yao kupitia ujumbe mfupi wa simu za kiganjani kama ifuatavyo;-
 
Huyu anasema,….Lisemwalo lipo na kama halijafika kwako, laja. Ni kweli pamoja na maendeleo ya haraka yaliyoletwa na simu kwa kuharakisha mawasiliano, wajanja wameweza kuwekeza sehemu mbalimbali ndani na nje. 
 
Na hii ni kutokana na ukweli kwamba mawasiliano yamekuwa rahisi ikilinganisha na miaka ya 1980, isipokuwa wajinga wachache wanaopotosha maana ya mawasiliano ya simu kwa sababu ya uvivu wa kufikiri.
 
Kweli asilimia 95 ya simu nchini hutumika kufikisha ujumbe wa kimapenzi aidha kwa mwanamke au mwanaume. Tuachane na mawazo mgando kwani mume au mke uliye naye anatosha uendako hakuna cha ziada kwani mapenzi ni yale yale tu (by Mwl. Bibiana A. Massawe, Tanga).
 
Mwingine…Simu siyo tatizo, kikubwa ni matumizi mabaya yameleta matatizo katika ndoa kwa kuwa wanandoa wanaweza kukosa uaminifu na kujikuta kwenye matatizo kimahusiano.
 
 Kwa upande wa marafiki pia inabidi kuwe na uchaguzi wa marafiki wema. Kuhusu utajiri au umasikini katika uhusiano watu wengine wanavuruga uhusiano wao kwa kuendekeza tamaa.
 
Nimependa sana hii makala kuhusu simu, kama mimi binafsi imenivuruga sana ndoa yangu, kwani huyu mwenzangu bora asingelikuwa na mawasiliano angalau na; Wengine ni wa zamani na wako kwa waume zao, wengine ndiyo hawa dada zetu wa Tanga. Yaani dada yangu nimezingirwa na mamluki wa ndoa. 
 
Wakati alipokuwa anacho yote hayakuwapo na nikihoji naambiwa ushamba wa mapenzi. Lakini ya watu wengine yuko mstari wa mbele kukosoa na kuona wenzie ndio wahuni au ambao hawajatulia kwenye ndoa zao. 
 
Huyu ana unafiki kuwa yeye ni msafi. Ama kweli simu zinachangia kuharibu ndoa za watu. (Ni mimi mwathirika kutoka Zanzibar, Nungwi).
 
Kwa wale ambao hawako kwenye ndoa hujikuta wakichangia mabwana/mabibi, kisa tu amepata namba ya simu ya shemeji yake.
 
Ninacho kisa cha binti mmoja aliye na rafiki yake wa kike. Baada ya kumpata kijana akawa kila anapogangana naye haachi kumhadithia rafiki yake, mfano eti leo tumetoka na shemejio, kumbe anayemsimulia anamuwinda yule kijana.
 
Siku moja akiwa binti amelala, rafiki yake akachukua simu yake akatafuta namba ya kijana akaihifadhi. Kulipokucha akaanza kumtumia ujumbe akitaka  wakutane na kweli alifanikiwa na kuanza mahusiano ya siri bila binti kujua. 
 
Na kibaya zaidi, huyu shoga wa binti kajaliwa haswa umbo na uzuri kwa jumla. Kijana hakuweza kuruka mtego. Sasa anti hizi simu kweli zitatuponyesha. Na hili gonjwa la ajabu tunaponea wapi? 
 
Mwingine anasema;....Asante mada zako nazifuatilia sana. Ndoa ilikuwa enzi za zamani wakati kukiwa hakuna pesa nyingi kama ilivyo sasa. Pesa imeharibu penzi na ndoa(Raster Tizo, Jozi Africa Kusini).
 
…Ukweli wapo wanaume ambao yeye akiwa na hela zinamsumbua, dharau zinakuwa nyingi kwenye ndoa. Yeye muda wote anakuwa buzy na wanawake, starehe nyingi kukicha tu ujumbe za simu (sms) zinaingia hapo tena atajifanya anawahi kazini. Mimi naona simu pamoja na hela zinaharibu sana ndoa (naitwa Moleni nipo Buguruni).
Chanzo:nipashe
CHANZO:NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!