Thursday, 1 February 2018

Magufuli ataka majaji wanaotumia likizo nje kuchunguzwa


Rais John Magufuli ameeleza kushangazwa na vibali vya ruhusa ziombwazo na majaji zikionyesha kuwa wanaenda nje ya nchi na familia yao kwa ajili ya likizo.


Akizungumza katika kilele cha Wiki ya Sheria jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi, Rais amemwagiza Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma kufuatilia suala hilo huku akijiuliza wanawezaje kujigharamia kwa siku 28-30 wakiwa Afrika Kusini, Uingereza na nchi nyingine huku kipato chao akiwa anakijua.
Ameeleza kuwa watumishi wengine hutumia siku za likizo kwenda vijijini kwa wazazi wao, lakini wengi wa majaji anaochukua likizo huenda nje ya nchi kwa siku nyingi na kuhoji anayewagharamia.
Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amewaomba wadau wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia (WB) kusaidia mhimili wa mahakama kwani unakabiliwa na changamoto kadha wa kadha ikiwemo magari na miundombinu mingine.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!