Februari 11, 1990, Nelson Mandela aliachiwa huru kutoka gerezani alikokuwa amefungwa kwa miaka 27, kwa kufanya harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.
Fahamu kwamba Nelson Mandela licha ya kutumia muda mwingi wa maisha yake kupigania haki na uhuru wa watu wa Afrika kusini, alitawala nchi hiyo kwa miaka 'mitano' tu tangu awe Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment