Leo February 20, 2018 nakusogezea stori ya Kimahakama kumhusu Mkazi wa Goba Matosa Ammy Lukole (49), anayedaiwa kumuua mkewe, shemeji yake na mtoto wake amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.
Lukole amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Kevin Mhina na Wakili wa Serikali, Masini Musa, ambapo amedai mshtakiwa ana makosa matatu.
Inadaiwa kwamba mtuhumiwa anayedaiwa kuwa Mhasibu kutoka Hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya, alitenda kosa hilo January 4, 2018 nyumbani kwake Goba Matosa.
Anadaiwa kumuua Pendo Makale, (mkewe), alimuua Magreth Samwel (shemeji yake) na pia alimuua Joshua Ammy (mtoto wake).
“Ulitenda kosa hilo kinyume cha kifungu sheria namba 196, cha mwenendo wa makosa ya jinai kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002,” -Wakili Musa.
Baada ya kusomewa maelezo ya kosa hilo, Wakili Musa amedai upelelezi bado haujakamilika ambapo Hakimu Mhina amesema mtuhumiwa hawezi kudhaminiwa pia hapaswi kujibu kitu chochote kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Mtuhumiwa amerejeshwa Mahabusu hadi March 6, 2018 kwa ajili ya kesi kutajwa.
No comments:
Post a Comment