Monday, 19 February 2018

Familia ya Wanandoa Waliokamatwa China naDawa za Kulevya Wafikiana Matunzo ya Mtoto


Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Daniel Masunzu amesema familia mbili za wanandoa Baraka Malali na Ashura Mussa zimekubaliana mtoto atunzwe na babu yake Hashim Mbarouk.


Wanandoa Baraka na Ashura walikamatwa Januari 19,2018 nchini China wakiwa na mtoto wao mwenye umri wa miaka miwili na miezi tisa wakituhumiwa kupatikana na dawa za kulevya.

Mbarouk ni babu upande wa mama aliyempokea mtoto huyo aliporejeshwa nchini Februari 14,2018.

Masunzu akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 19, 2018 baada ya majadiliano na pande hizo mbili, amesema muafaka umepatikana mtoto kuwa chini ya familia ya Mbarouk na Zuhura Nyangasa ambaye ni bibi yake upande wa mama.

“Familia zote mbili zimekubaliana kuhusu hatua hii. Mtoto kukaa upande wa Mbarouk haina maana kwamba matunzo watayatoa wao peke yao, bali ndugu wengine wana jukumu la kuendelea kufanya mawasiliano na mtoto kwa ajili ya matunzo,” amesema Masunzu.

Akizungumza kwa niaba ya familia hizo mbili, Wile Stanford ambaye ni kaka wa Malali amezishukuru Serikali za Tanzania na China kwa kumrejesha salama mtoto huyo.

Amesema wazazi wa pande zote mbili wamefikia makubaliano mazuri kuhusu matunzo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!