Friday, 9 February 2018

Dawa za kulevya zakamatwa bahari ya Hindi



Vikosi vya ulinzi wa majini vya nchini Australia vimekamata kilo 1,365 za dawa za kulevya aina ya heroine kipindi cha kati ya Januari na Februari, kupitia bahari ya Hindi eneo la Tanzania.



Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 8, 2018 bungeni mjini Dodoma, kamishna mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Sianga amesema kati ya kiasi hicho, kilo 965 zimekamatwa Februari 2018 na kwamba,katia ya hizo 650 zilikuwa ziingizwe nchini.
Amesema mamlaka hiyo imekuwa ikivunja mitandao ya dawa za kulevya na kwamba, kilo 200 zilikamatwa katika gari la Mtanzania mpakani mwa
Msumbiji na Afrika Kusini.
“Tunawaambia hata kama wakikimbilia nchi nyingine tutawakamata tu, haiwasaidii,”amesema.
Kuhusu mbinu mpya ya watumiaji dawa za kulevya, Sianga amesema baada ya dawa za kulevya kuanza kuadimika sasa wanatumia ugoro na gundi.
Amesema mamlaka hiyo inafanya utafiti kuchunguza kiasi cha Nicotine kilichopo katika vitu hivyo.
Pia, amebainisha kuwa watumiaji hao hutumia dawa zinazolevya ikiwamo Ketamin, Valium, Tramadol, Pethidene na Merphine Powder.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!