Thursday, 11 January 2018

Treni ya abiria chupuchupu mlipuko wa gesi Dar

Related image
Picha haihusiani na Habari husika

BOMBA la gesi lililolipuka juzi kwenye kituo cha Buguruni kwa Mnyamani, Dar es Salaam, lililipuka ikiwa ni dakika tano tu baada ya treni ya abiria ya Shirika la Reli (TRL) inayotoa huduma za usafi ri jijini Dar es Salaam, kuondoka kwenye eneo hilo.


Kulipuka kwa bomba hilo kulisababisha taharuki hasa kwa wakazi wa eneo hilo na maeneo jirani yakiwamo Vingunguti na Tabata huku wezi wakitumia nafasi hiyo kuiba mali za watu katika majumba na maduka ambayo wahusika wake waliyaacha wazi wakiwa kwenye harakati za kuokoa maisha yao dhidi ya mlipuko huo.
Gazeti hili lilifika kwenye eneo la tukio saa moja na dakika tano usiku, ikiwa ni dakika takribani 25 baada ya moto huo kuzuka na kushuhudia watu kadhaa wakiendelea kuhamisha vitu vyao hasa wale walio eneo la mbali kidogo na eneo lilipolipukia bomba.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo wa Mji Mpya, Rahma Sufiges, aliliambia gazeti hili kuwa licha ya kusikitishwa na mlipuko huo lakini anashukuru Mungu kwa kuwa umetokea ikiwa ni dakika tano baada ya treni iliyojaza abiria kutoka eneo hilo.
"Pengine hali ingekuwa ni mbaya zaidi kwa kuwa ilikuwa imeshusha na kupakia watu wengi na kuondoka kwenye eneo hilo na hapo ndipo mlipuko ulipotokea pengine hali ingeweza kuwa mbaya zaidi kwa kuwa wangepata taharuki kubwa, lakini pia ninashukuru katika tukio hili la mlipuko hakuna aliyepoteza maisha," alisema Sufiges.
Akizungumzia zaidi kuhusu mlipuko huo uliosababishwa na moto wa wauzaji wa bidhaa za vyakula kwenye eneo hilo, ikiwa ni baada ya mafundi wa Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco) kulichimba bomba la gesi wakati wakiendelea na utandazwaji wa mabomba ya maji.
Alisema, baada ya kutokea kwa mlipuko akishirikiana na askari polisi wa eneo hilo waliwahi ili kutoa msaada na kukuta moto huo umeshaanza kuunguza nyumba moja iliyokuwa jirani, kulipua transfoma na unguza nyumba chache. Jana mchana Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema alitembelea eneo hilo na kuagiza askari kuimarisha ulinzi kwa wakazi wa eneo hilo huku akiihakikishia msaada kutokea mfuko wa maafa wa wilaya familia hiyo iliyounguliwa nyumba.
Pia alipiga marufuku wafanyabiashara kuendelea kufanya biashara kwenye eneo la karibu na bomba la gesi huku akiliagiza Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua mafundi wa Dawasco waliosababisha uharibifu wa bomba hilo. Ofisa Habari wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Francis Lupokela alitoa mwito kwa wananchi na kampuni kuheshimu alama zinazotahadharisha kuhusiana na usalama wa mabomba hayo.
Alisema: "TPDC ambao ni wenye dhamana ya gesi tumeguswa na kilichotokea lakini tunawapa pole waathirika wa tukio hili na tunaagiza watu na kampuni kuheshimu alama zinazotahadharisha kuhusiana na usalama wa gesi." Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy inayosimamia usafirishaji wa gesi hiyo, Andy Hanna alisema huduma ya usafirishwaji wa gesi hiyo utarejea leo na kuongeza kuwa takribani kampuni 20 zimeathiriwa na tukio hilo.
Alisema, kwa sasa hawawezi kusema hasara halisi iliyosababishwa na tatizo hilo, ila alibainisha kuwa wamenunua vifaa vipya mbalimbali katika kuhakikisha urejeshwaji wa huduma hiyo, na kuwataka watu kuheshimu alama zinazotahadharisha kuhusiana na upitishwaji wa gesi hiyo.
Nalo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Temeke, limewataka wahandisi na wakandarasi wanaojihusisha na ujenzi wa miundombinu ya barabara na umeme wa majengo kutoa taarifa katika ofisi za Zimamoto kwa lengo la kuepusha madhara ya moto yanayoweza kujitokeza.
Kamanda wa jeshi hilo, Mkoa wa Temeke, Leiser Lospy alisema hatua hiyo imelenga kukabiliana na tatizo la ghafla la moto kama lililojitokeza juzi eneo la Buguruni, ambalo kimsingi athari yake wangeweza kuidhibiti mapema. Akizungumzia tukio hilo, Lospy alisema, kimsingi lingeweza kuzuilika au madhara yake kupungua kama Dawasco wengetoa taarifa mapema Zimamoto kuhusu kazi hiyo, hatua ambayo ingewawezesha wao kufika mapema na kuchukua tahadhari.
"Ni vyema hawa wenzetu wakawa wanatoa taarifa mapema kwa Jeshi la Zimamoto, kwa mfano kama wangekuwa wametupa taarifa za zile tukio mapema tungeweza kuwa nao hado wanapomaliza kazi yao ili kukabiliana na hatari yoyote ambayo ingejitokeza," alisema Lospy. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Kapuulya Musomba, alisema moto huo usingetokea kama Dawasco wangechukua tahadhari kabla ya kuanza shughuli zao katika eneo hilo.
Alisema, utaratibu uliopo mamlaka yoyote inapaswa kuomba kibali cha kupitisha bomba eneo lolote mahali ambalo bomba la gesi limepita ili hatua za tahadhari ikiwemo kuwapa mtaalam ichukuliwe, jambo alilosema halikufanywa na Dawasco. Aidha gazeti hili lilipomtafuta Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Cyprian Luhemeja ili kupata ufafanuzi wa masuala hayo, hakuweza kupatikana baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!