Sunday 21 January 2018

Serikali yazifutia usajili meli 2 zilizonaswa na dawa za kulevya

BAADA ya agizo la Rais John Magufuli la kusisitiza marufuku ya michango shuleni, wakuu wa mikoa na wilaya nchini wamecharuka na kuwataka maofi sa wa elimu kuchukua hatua dhidi ya walimu walioukiuka agizo hilo.

Wiki hii, Rais Magufuli aliwaambia mawaziri wawili, wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako na wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo kuhakikisha wanawachukulia hatua wote wanaotoza michango shuleni baada ya serikali kutoa elimu bure hadi kidato cha nne.
Mkoani Iringa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amekutana na walimu wakuu kutoka wilaya zote za mkoa huo na kuwataka kuandika kwake barua ya mkono wakieleza kama kuna michango katika shule zao.
“Katika barua hizo nataka kila mmoja aeleze kama katika shule yake kuna aina yoyote ya mchango uliopigwa marufuku, sababu za kuwepo kwake, aliyeidhinisha, kiasi cha mchango na kwa ajili ya kazi gani,” alisema juzi wakati akizungumza na walimu wa wilaya za Iringa na Kilolo kabla hajaelekea wilayani Mufindi kwa lengo hilo hilo.
Alisema baada ya kupokea barua hizo kutakuwepo na utaratibu wa kupita katika kila shule na kuzungumza na kamati, bodi za shule na jamii ya wanafunzi ili kujiridhisha kama taarifa zilizotolewa ni za kweli au siyo za kweli.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro ametoa rai kwa waratibu wa elimu kwenye kata mbalimbali za Jiji la Arusha kutatua changamoto za elimu badala ya kukaa maofisini na kuletewa taarifa za watoto kufukuzwa shule au kuchangishwa michango iliyopigwa marufuku na serikali katika utoaji wa elimu bora.
Aidha, wazazi na walezi wenye watoto wanaosoma shule za msingi na sekondari ambao wanaendelea kutozwa fedha za michango iliyopigwa marufuku shuleni wameaswa kutoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia, maofisa elimu sanjari ili kuwachukuliwa hatua wahusika.
“Hii haikubaliki na nawaomba wazazi na walezi wa watoto wawafichue walimu hao wanaochangisha michango isiyostahili maana kwa nini mtoto achangie kununua tanki la kuhifadhia maji wakati hakuna makubaliano ya wazazi halafu nyie waratibu wa elimu Kata mmekaa ofisini tu nasema hapana na sitakubali kila mtu asome waraka wa elimu unasemaje,” alieleza.
Daqqaro alisema hayo alipozungumza na walimu wakuu wa shule za msingi, sekondari na waratibu wa elimu kata kwenye kikao kwa kukumbushana wajibu wa kazi zao na kuepuka michango isiyostahili kwa wanafunzi.
Alisema baadhi ya waratibu wa elimu kata wamekuwa na tabia ya kuchukua taarifa za elimu kwa ripoti za walimu darasani badala ya kupita shuleni kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa michango isiyostahili mashuleni.
Imeandikwa na Veronica Mheta (Arusha) na Frank Leonard (Iringa).

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!