Monday 22 January 2018

Salum Njwete “SCORPION” ahukumiwa Jela miaka 7

January 22, 2018 kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala imetolewa hukumu ya Salum Njwete maarufu kama ‘SCORPION’ ambae amehukumiwa miaka 7 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumjeruhi na kumsababishia upofu Said Mrisho.


Scorpion ambae sakata lake lilikua kubwa mpaka Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kuingilia kati na kumsaidia Said Mrisho mwaka 2016 ambae kwa sasa hana uwezo wa kuona tena, ameamuriwa pia na Mahakama kulipa faini ya MILIONI 30 ambayo atapewa Mrisho kama fidia.
Pia Mahakama hiyo imemuachia huru Scorpion katika kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha, Hukumu imesomwa na Hakimu Mkazi Frola Haule na kulikuwa na Mashahidi 10.
Hakimu Haule amesema katika hukumu hiyo Mahakama ilijikita sehemu kuu tatu ikiwemo kama mlalamikaji Said Mrisho  amepata majeraha ya hatari ama lah pamoja na kama Scorpion alitumia unyang’anyi wa kutumia silaha.
“Faini ilipwe wakati unatumikia kifungo, pia ni ruksa kukata rufaa kwa upande wowote kama haujaridhika,” – Hakimu Haule
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Njwete anaetetewa na wakili Juma Nassoro anaidaiwa September 6, 2016 saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Dar es Salaam, aliiba cheni ya Silva yenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000.
Vingine ni simu ya mkononi na fedha taslimu Shilingi 330,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh 474,000 mali ya Said Mrisho Said huku ikidaiwa kabla na baada ya kutekeleza tukio hilo, Scorpion  alimchoma Mrisho sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo machoni, tumboni na mabegani ili kurahisisha kupata mali hizo.
Said Mrisho ameonekana kutoridhishwa na hukumu hiyo ya miaka 7 na kusema ni ndogo hivyo atapeleka ombi lake kwa Rais Magufuli.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!