Sunday 21 January 2018

BINTI MWENYE UVIMBE BEGANI AFARIKI DUNIA AKITIBIWA

Maria Amrima Sandalu (17) mkazi wa Mtwara, aliyekuwa na uvimbe begani amefariki dunia akipatiwa matibabu Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI). Mariam ambaye ni mkazi wa Masasi mkoani Mtwara, amefariki dunia leo alfajiri akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI).


Binti huyo ambaye alitakiwa kufanyiwa upasuaji Muhimbili mwaka mmoja uliopita wakati huo uvimbe ukiwa bado mdogo, alitoweka baada ya kwenda katika tiba za asili kabla ya kurejea hospitalini hapo Januari 3 mwaka huu, baadaye kuhamishiwa katika taasisi hiyo. Mkurugenzi wa ORCI, Julius Mwaiselage amethibitisha kifo hicho, kwamba taasisi hiyo inaandaa taarifa kamili.
Binti huyo ambaye alitakiwa kufanyiwa upasuaji Muhimbili mwaka mmoja uliopita wakati huo uvimbe ukiwa bado mdogo, alitoweka baada ya kwenda katika tiba za asili kabla ya kurejea hospitalini hapo Januari 3 mwaka huu, baadaye kuhamishiwa katika taasisi hiyo.
Awali jopo la madaktari bingwa kutoka vitengo vitatu vya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Ocean Road, waliungana kwa pamoja kuangalia uwezekano wa kumtibu na kuokoa maisha yake baada ya tiba ya upasuaji kushindikana. Waziri Ummy amesema inasikitisha kwani msaada wa Watanzania haukuweza kuokoa maisha yake.
Tutaongeza jitihada zaidi kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwahi hospitalini kufanyiwa uchunguzi na kuzingatia maelekezo ya madaktari wanayopewa ikiwamo kuanza matibabu mara moja na si kwenda kukaa nyumbani na mgonjwa,” amesema Waziri Ummy ambaye hivi karibuni alimtembelea Mariam hospitalini kumjulia hali.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!