Rais Trump amefanya maamuzi ya kihistoria ya kuipindua sera za miaka mingi ya Marekani kwa kuutambua mji wa Yerusalem kuwa ndio mji mkuu wa Israel.
Rais huyo pia ametangaza kuwa Ubalozi wa Marekani utahamishwa kutoka katika eneo la sasa la Tel Aviv kwenda Yerusalem. Amesema kuwa uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za kuleta amani katika eneo hilo la mashariki ya kati.
Trump amesema uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za dhati za kuleta amani ya kudumu bali inataka kutafuta suluhu ya mgogoro wa miaka mingi kati ya Israel na Palestina ambao .Marekani haifungaman na upande wowote na kuingilia mipaka ya Israel na mamlaka zake ,na hatuko tayari kuingilia katika migogoro yao ,hayo ni mambo yao wenyewe.
Huku kwa upande wake Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesikitishwa na maamuzi ya rais Trump na kudai kuwa Marekani imepoteza haki ya kusimamia hatua ya kupatana kwa amani ambayo imekuwa ikitafutwa miongo kadhaa iliyopita.
Huku waziri mkuu wa Israel ,Benjamin Natanyau ameonekana kuunga mkono hatua ya rais Trump kwa kuelezea kuwa ni maamuzi ya kihistoria licha ya kuwa wapalestina wamemkosoa na huku Uingereza na nchi nyingine wanachama wa baraza la usalama wa umoja wa mataifa wameitisha kikao cha dharura ili kujadili maamuzi yaliyofanywa na rais Trump
No comments:
Post a Comment