Saturday, 9 December 2017

RC ataka waliotia mimba wanafunzi 20 kukamatwa

MKUU wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo ameitaka polisi mkoani humo kuwakamata watu waliowatia mimba wanafunzi 20 ambao walishindwa kufanya mitihani yao ya kumaliza darasa la saba mwaka huu.


Aliyasema hayo mjini Kibaha wakati wa kikao cha bodi ya uteuzi wa wanafunzi waliofaulu na wanaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2018 na kuongeza kuwa wanafunzi hao wa kike ndiyo walioshindwa kufanya mitihani yao ya kumaliza darasa la saba kutokana na kupata ujauzito kwenye mkoa huo.
"Naagiza polisi kuwakamata watu hao waliowatia mimba wanafunzi wakashindwa kufanya mitihani yao ya kumaliza darasa la saba mwaka huu," alisema Ndikilo na kuongeza kuwa sheria ziko wazi kwa wanaowatia mimba wanafunzi hivyo wahusika hao wakamatwe wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma hizo.
Alisema haiwezekani kuwakalia kimya wahusika kwani wamewaharibia maisha watoto hao ambao ndoto zao zimeyeyuka kwa kukatishwa na watu wasio na utu hivyo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!