Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemhukumu Mkazi wa Kijiji cha Itenka, Wilaya ya Mpanda kifungo cha miaka 20 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kukutwa na nyama ya kiboko zaidi ya kilo 110 yenye thamani y ash milioni 2.3.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga Ntengwa ametoa hukumu hiyo leo Ijumaa Desemba 8, baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali, Flavian Shio.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Chiganga amesema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka ambao ulikuwa na mashahidi watano na mshitakiwa hakuwa na shahidi yeyote.
“Mahakama pasipo shaka yoyote imemuona mshtakiwa ana hatia kupitia Kifungu cha Sheria Namba 86 (1) na (2) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009,” amesema Hakimu Chiganga.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Omary Maganga alitenda kosa hilo Oktoba 10 mwaka jana ambapo alikamatwa akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi akiwa na nyama ya kiboko yenye uzito wa kilo 118 yenye thamani ya Sh milioni tatu.
MTANZANIA
No comments:
Post a Comment