Saturday 16 December 2017

CHAKULA CHA USIKU HUCHANGIA ZAIDI KUONGEZEKA UZITO NA UNENE




Tatizo la uzito mkubwa sasa limekithiri sana na watu wanahangaika kupata matibabu yake kwa mafanikio madogo sana. Kinachowakwamisha wengi ni kutoelewa misingi ya uzito mkubwa wa mwili na kuhangaika na mambo mbalimbali ambayo wanayasikia huku na kule bila kupata uhakika wa ukweli na upotofu wake.

Leo jua mambo mawili kisha yafanyie kazi vizuri:
1. Uzito na unene huongezeka kutokana na kukua kwa mwili na/au kuhifadhiwakwa chakula cha ziada katika mtindo wa mafuta mwilini
2. Kula chakula zaidi ya kile kinachotakiwa na kutojishughulisha vya kutosha kwa mazoezi na shughuli za kutumia nguvu huchangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka uzito na unene


CHAKULA CHA USIKU
Kwa wengi wetu usiku hatufanyi kazi za kutumia nguvu nyingi na kuweza kutumia vyakula tunavyokula usiku. Matokeo yake ni chakula hicho kuhifadhiwa mwilini kama mafuta na kuchangia kuongezeka uzito na unene.
KUTOJISHUGHULISHA AU KUTOFANYA MAZOEZI
Kutofanya mazoezi pamoja na kutojishughulisha na kazi zinazotumia nguvu hufanya mwili kushindwa kutumia chakula cha ziada kilichohifadhiwa mwilini na matokeo yake kinaendelea kuongezeka siku hadi siku na kufanya uzito na unene kutopungua au kuongezeka zaidi
MAMBO YA KUFANYA ILI KUDHIBITI UZITO NA UNENE
Mambo makubwa zaidi ni mawili tu:
1. Dhibiti kiasi cha chakula unachokula
Jua kwa usahihi kiasi cha chakula kinachotakiwa na mwili wako kulingana na umri wako, jinsia yako, shughuli zako nk
Punguza ulaji wa sukari na vyakula vya wanga.
Hapa ndo kwenye kitovu cha uzito mkubwa na unene. Na ndio mtego ambao umewanasa watu wengi sana huku wenyewe wakiwa hawajui wamenasa wapi. Ni kwa bahati mbaya sana kwamba sukari hupatikana kwenye vyakula vingi sana na watu wengi zaidi hupenda vyakula hivyo na huvila kwa wingi zaidi.
Punguza kabisa kiasi na ulaji wa sukari na vyakula vya wanga kama vile wali, ugali, mihogo, viazi, chipsi na kadhalika
2. Shughulisha zaidi mwili wako na ufanye mazoezi ya kutosha
Hii itasaidia sana kutumia mafuta na vyakula vilivyohifadhiwa mwilini mwako ambao ndio huo unene na mafuta uliyonayo. Fanya mazoezi ya viungo na ushughulishe mwili wako. Tembea, fanya kazi za mikono, cheza mpira na uruke kamba. Hata kama wewe ni boss basi jitahidi sana kuweka uboss pembeni maana ndio unakucost.
ANZA SASA. NA USIACHE MPAKA UFANIKIWE
Mara nyingi mwanzo ni mgumu sana. Anza kidogo kidogo ili usije ukashindwa ghafla au ukajisikia vibaya sana. Punguza kiasi cha chakula kidogo kidogo, punguza ulaji wa vyakula na unywaji wa vinywaji vyenye sukari. Unapoweza kuacha acha kabisa na mwili wako utatumia kilichopo tumboni.






No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!