“TAARIFA kutoka vituo mbalimbali vya afya vilivyopo katika Manispaa ya Mpanda zinaonesha kuwa wasichana wapatao 624 wenye umri chini ya miaka 18 wamejifungua katika vituo vinavyotoa huduma za afya katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.”
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga, alisema hayo katika uzinduzi wa Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia uliofanyika kimkoa katika Viwanja vya Saba Saba, katika Kijiji cha Kabungu wilayani Tanganyika.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga aliwataka wanawake wenye kasumba ya kuwapiga waume zao, waache kwani wanawaaibisha wanawake wengine nchini. Muhuga yeye alisema, Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa 2015 na 2016 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, unaonesha Mkoa wa Katavi unaongoza kitaifa kwa mimba za utotoni.
Alisema ilibainika kuwa, asilimia 45 ya wasichana wenye umri wa miaka kati ya 15 na 19 wameshazaa huku asilimia 33.3 wakiwa na mtoto aliye hai angalau mmoja. Alisema mashauri 401 ya ukatili yalihusu ukatili wa kimwili, 66 kingono, 262 kisaikolojia na 447 yalihusu kutelekeza watoto na familia zao. Ukatili wa kimwili na kingono ulifanywa na wanaume
No comments:
Post a Comment