Wednesday, 8 November 2017

Wanafunzi sita wafariki kwa bomu Kagera, 41 wajeruhiwa

Taharuki, huzuni na majonzi makubwa yameukumba Mkoa wa Kagera baada ya kutokea vifo vya wanafunzi sita kutoka katika shule ya Msingi ya Kihinga iliyopo wilayani Ngara vilivyosababishwa na mlipuko wa bomu wakati wanafunzi wakiwa mstarini.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Augustino Ollomi akithibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema wanafunzi wengine 24 walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Misheni ya Rulenge, wilayani humo.
Kwa mujibu wa Kamanda Ollomi, mwanafunzi mmoja alikuja mstarini akiwa na chuma kwa lengo la kukipeleka kukiuza kwa mnunuzi wa vyuma chakavu, jirani na shule hiyo. Kabla ya wanafunzi hao kutawanyika mstarini hapo, mwanafunzi huyo akidhani ni chuma chakavu alichobeba kumbe ni bomu, lilimlipukia na kusababisha vifo hivyo.
Uchunguzi kutokana na tukio hilo unaendelea.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!