Monday, 13 November 2017
Wafanyabiashara wauawa na kutupwa ziwa Victoria mkoani Mara
MARA: Miili ya watu watatu wanaodaiwa kuwa ni wafanyabiashara imekutwa imetupwa ndani ya Ziwa Victoria huku miguu na mikono ikiwa imefungwa kwa kamba na kuwekewa mawe
Wananchi wanadai ndani ya siku tatu wameshuhudia miili mitano ikiwa imefungwa kwa staili hiyo na kutupwa ziwani
Kamanda wa Polisi mkoani Mara Kamishna msaidizi Jafari Mohamed amethibitisha kupata taarifa hizo kutoka kwa askari wake na uchunguzi unaendela, huku akiwataka waliopoteza ndugu zake kufika Hospitali ya Rufaa mjini Musoma ili kutambua miili hiyo
JMF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment