JESHI la polisi nchini limesema hadi sasa hakuna watu waliojitokeza kutambua au kulalamika kwamba wamepoteza ndugu zao kufuatia kuwapo kwa idadi kubwa ya miili inayookotwa maeneo mbalimbali.
Miili hiyo imekuwa ikiokota ikiwa imewekwa kwenye viroba na mingine ikiwa imefungwa mawe makubwa na kamba. Mkuu wa Jeshi hilo nchini (IGP), Simon Sirro alisema kumekuwepo na changamoto ya kuwapata watu wanaodai kupotelewa na ndugu zao, ili Polisi waweze kufuatilia kwa karibu kadhia hiyo.
Alisema Jeshi hilo lilitoa taarifa za kuokotwa kwa miili hiyo katika maeneo mbalimbali, hususani katika jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya upelelezi wa vinasaba (DNA) lakini hawajaona mtu yeyote aliyejitokeza kwa ajili ya kutambua mwili wowote ule.
Sirro alisema kutokana na hali hiyo, jeshi hilo linaendelea kupeleleza na baada ya hapo utaratibu mwingine uweze kufuatwa. “Kimsingi bado hakuna mwili hata mmoja uliotambuliwa wala ambaye amefika kutambua, hivyo utaratibu mwingine unaendelea kwa aliyeshindwa
No comments:
Post a Comment