MH A D - HIRI wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Nancy Marobhe amesema katika utafiti alioufanya kuhusu shida ya maji vijijini amebaini mbegu za mlonge na mkeketa zikisagwa zina uwezo wa kusafisha maji na kuwa masafi.
Profesa Marobhe alisema hayo mwishoni mwa wiki kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya ushirikiano wa masuala ya utafiti baina ya Tanzania na Sweden yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema utafiti huo aliufanya katika kata ya Magojoha, Singida Vijijini ambapo alibaini kuwa wanawake wa eneo hilo walikuwa wakisafisha maji machafu kwa ajili ya kunywa na matumizi mengine kwa kutumia mbegu hizo bila kufuata vipimo sahihi.
Profesa Marobhe alisema aliamua kufanyia tafiti mbegu hizo ili ziwe na matumizi sahihi kwa watumiaji kwa kuwa ilikuwa ndiyo njia pekee ya kuwasaidia kwani visima vilivyokuwepo vingi vilikuwa vimeharibika kutokana na ukosefu mzuri wa uangalizi.
Alisema pia alipowafuatilia alibaini hata wanapotumia mbegu hizo bado maji yalikuwa siyo safi, yana matope ndipo alipoamua kufanya utafiti wake alikuja na matokeo chanya.
“Tunahitaji teknolojia ya asili ili teknolojia ioneshe matokeo kwa watu wa vijijini inabidi tuungane wadau wote na serikali ili kuisambaza hiyo teknolojia,” alisema na kuongeza kuwa alipata matokeo mazuri maabara ambayo yatawasaidia wanakijiji kupitia mbegu hizo za kusafishia maji machafu.
No comments:
Post a Comment