Thursday, 30 November 2017

Mambo yatakayoboresha maamuzi yako ya kila siku - Nguvu ya Maamuzi.



1. Jithamini
Thamini afya yako, muonekano wako,mambo yako. Kujithamini ikiwa ni moja kati ya vipaombele vyako muhimu hautafanya maamuzi yoyote yale yenye lengo la kuharibu thamani yako, watu wanaothamini afya zao na mionekano yao hawathubutu kamwe kutumia pombe,sigara, hawali ovyo, wana mipaka na uchaguzi sahihi wa vyakula  pia hula kwa kiasi na kufanya mazoezi.  


Watu wanaojithamini hawawezi kuuza thamani yao kwa pesa iwayo yoyote ile, hujitengenezea misimamao thabiti yenye kulinda thamani zao maandiko yanatusisitiza jinsi tunavyopaswa kujithamini kwa sababu sisi ni wathamani  uthamani wetu ulimfanya Mungu aifanye miili yetu kuwa hekalu lake  “Je hamjui kuwa miili yenu ni hekalu la roho mtakatifu?” (1wakorinto 6;19-20) Uthamani wetu ulimfanya Yesu amwage Damu yake ili atukomboe (Petro1;18-19) “mlikombolewa kwa dami ya thamani”  uthamani wetu haulinganishwi na kitu chochote, ama pesa iwayo yoyote ile kujithamini kutaboresha maamuzi yako ya kilasiku kwa sababu kunakutengenezea mfumo wa maamuzi ambao hautaruhusu kitu chochote kile chenye lengo la kuharibu thamani yako.

2. Jiwekee ratiba ya mambo ya kufanya kila siku na kuisimamia. 
Usifanye jambo ambalo hukulipanga. Usiende mahali ambapo hukupanga kwenda kwenye ratiba yako, uwe na ratiba ya kila ikionyesha muda wa kufanya kila jambo kwa siku husika, Muda wa kuomba omba kweli, Muda wa kusoma neno soma neno, Muda wa kukaa na familia yako hakikisha unafanya hivyo kweli, Muda wa kupumzika pumzika  Na muda wa kufanya kazi Fanya kazi kweli kweli.Hakikisha unakuwa na nidhamu ya hali ya juu kuheshimu ratiba yako kwa Kufanya jambo ambalo umelipanga hii  itakusaidia kuboresha maamuzi yako na kukuondolea hatari ya kufanya maamuzi mabaya kwa sababu  kuandaa ratiba kunakupa nafasi ya kutafakari jambo sahihi la kufanya na kwa nini ufanye hilo na si mengine.

3. Jiwekee malengo ya kutimiza kila siku kila wiki kila mwezi n.k
Hii itakuongezea kasi ya kukamilisha mambo yako  usiishie kupanga ni lazima pia ujikague  je umefanikisha yale uliyoyapanga kwa kiasi gani? kujiwekea malengo na mikakati ya kutimiliza malengo hayo kutasaidia mawazo yako na maamuzi yako kulenga zaidi kutimia kwa malengo hayo, hivyo kuboresha maamuzi yako ya kila siku, kuwa na malengo kunautengenezea mfumo wetu wa kufikiri vipaombele, hivyo kudhibiti mfumo wetu wa maamuzi kuelekea mafanikio ya  vipaombele vyetu jambo ambalo lina msaada mkubwa sana katika kuboresha maamuzi yetu ya kila siku.

4. Yafanye maono uliyonayo kuwa kama kipimio cha kila maamuzi unayotaka kuyafanya. 
Kama kioo cha ratiba unayojiwekea na kama mwongozo wa malengo tunayojiwekea;  Maamuzi yetu yalenge utimilifu wa maono yetu hii itakusaidia kugundua na kupangua kwa haraka jambo lolote lile linalokinzana na maono yako , maono yako yakutengenezee imani na msimamo thabiti,mambo haya yataboresha maamuzi yako kwa sababu kila maamuzi unayofanya yatakupa hatua zaidi ya kukaribia maono yako.

5. Pata Muda wa kutosha wa kusoma neno la Mungu. 
Ukamilifu na ubora wa maisha ya Mwanadamu upo katika kuenenda sawa sawa na neno la Mungu Mungu alimwambia Joshua kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako bali uyatafakari mchana na usiku ndipo utakapofanikiwa katika njia yako na ndipo utakapo sitawi sana, Neno la Mungu likikaa kwa wingi ndani yetu linaathili mfumo wetu wa kufikiri jambo hili linasababisha tufanye maamuzi sawa sawa na mapenzi ya Mungu. 

Nje ya Neno la Mungu kuna uharibifu maadiko yanatufundisha jinsi ambavyo tunapaswa kumtegemea Mungu wala si akili zetu wenyewe  kwa sababu ipo ile njia ionekanayo kuwa ni sawa machoni pa mtu lakini mwisho wake ni njia za mauti,  Akili zetu huelekea uharibifu hivyo ubora wa maamuzi yetu ya kila siku utategemea ni kwa kiasi gani ufahamu wetu na akili zetu zimeathiliwa na neno la Mungu.

6. Pata Muda wa kutosha wa kuomba. 
Kuomba ni njia ya kuwasiliana sisi na Mungu; ili tufanye maamuzi yaliyobora tunahitaji tujiweke karibu zaidi na Mungu kwa njia ya maombi tunapoomba tunaruhusu utawala wa Mungu kwenye mfumo wetu wa Maamuzi, tunapoomba Roho mtakatifu anatuongoza na kutufundisha, tunapoomba fahamu zetu zinapewa kuona kwa namna ya mwili na kwa namna ya Roho. 

Shetani hupanga mashambulizi na kuandaa mitego ya kutunasa na kutuangusha kupitia maamuzi yetu, pasipo kuomba ni rahisi sana  kufanya maamuzi yatakayokuingiza kwenye mtego wa shetani Tunapoomba Mungu anatupa hekima ya kuona mabaya na kujificha Maombi ni siraha itakayotusaidia kufanya maamuzi sahihi na kuboresha maamuzi yetu ya kila siku.

7. Usikae bila kitu cha kufanya.
Kuna msemo wa lugha ya kingereza unasema “an iddle mind is devils’ workshop” maana yake akili iliyokosa jambo la kufanya ni kiwanda cha shetani, Mungu alimuumba mwanadamu na kumpa kitu cha kufanya Akamuagiza mwanadamu ailime aitunze na kuipalilia bustani ya edeni. 

Kukaa bila kitu cha kufanya husababisha maamuzi yako kuwa kama bendela inayofuata upepo na kujiweka kwenye hatari ya kufanya maamuzi mabaya.

Kwa sababu hauna kitu cha kufanya hivyo chochote kitakachokuja kwenye akili yako na kupata ushawishi mkubwa ndicho utakachokifanya, Hii ni kwa sababu akili imekosa jambo maalumu la kufanya, Hivyo ili kuboresha maamuzi yako ya kila siku hakikisha unajiwekea ratiba inayokufanya kuwa bize Muda wako usipotee bure  bali utumie kikamilifu kwa kufanya mambo sahihi kwa wakati sahihi.

EMMANUEL MWAKYEMBE (MR. YOPACE)


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!