Thursday 5 October 2017

SABABU ZINAZOPELEKEA MTOTO KUTOKUCHEZA TUMBONI


Mama mjamzito huwa anaskia raha pale mtoto anapoanza kumpiga piga tumboni kwa mara ya kwanza. kucheza kwa mtoto kunafanya kuwa na mawasiliano mazuri kati ya mama na mtoto .Kwa wenye mimba ya kwanza mtoto ataanza cheza wiki ya 24 miezi (5-6), ila kwa wale walio zaa tayari mtoto mmoja au zaidi  wanaskia mtoto akicheza akiwa wiki ya 18-22 mapema kidogo.

Sababu zinazopelekea mtoto kutocheza tumboni:

Mtoto kukosa nguvu za kutosha kutokana na lishe mbaya ya mama yake,

:Mtoto hapati hewa ya kutosha kutoka kwenye placenta

:Mtoto kuwa mdogo sana na uzito mdogo nayo unamfanya ashindwe kucheza au akacheza kwa mbali sana na kukufanya wewe usimskie kama anacheza.


:Mama anapokuwa na maradhi au matatizo ya kiafya,  hudhoofisha afya ya  mtoto na kukosa nguvu


:Mama anapokuwa amechoka sana kwa safari au kazi ngumu ,mtoto nae anakuwa anachoka na kuhitaji kupumzika na huwa kimya sana


:Mama anapotembea sana au kusimama kwa muda mrefu,kuna mfanya mtoto analale na kumfanya asicheze .


Njia za Kumfanya Mtoto acheze tumboni:

Mama anapohisi mtoto yupo kimya anaweza

:Kunywa maji baridi sana

:Kunywa juice

:kaa sehemu yenye makelele kama ya radio,tv au washa vacuum cleaner

:Kula chakula au snacks -ataanza kucheza

:Lala ulalie ubavu  wa kushoto

:Kaa chini na unyooshe miguu juu ya kitu


Iwapo ukatumia njia zote hizo na bado yupo kimya ni vizuri ukawahi hospital  ,iyo ni ishara mbaya.


SHUKRAN KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!