Friday 6 October 2017

RC MAKONDA KUSAIDIA WAGONJWA 1,000 KUPATIWA MATIBABU YA MACHO NA MIWANI BURE


Mwendelezo wa Zoezi la Upimaji wa Afya Bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye Matatizo ya Macho linaendelea na sasa ni Huduma ya Matibabu ya Macho kwa Wananchi waliobainika kuwa na Matatizo ya Macho kwenye Kampeni ya RC Makonda ya Upimaji wa Afya Bure.


Zoezi hilo ni kufuatia ahadi iliyotolewa na Jumuiya ya Waislamu wa Dhehebu la Khoja Shia Ithnasheri Jamaat K.S.I.J iliyojitolea kumuunga Mkono RC Makonda kwa kujitolea Matibabu ya wagonjwa watakaobainika kuwa na matatizo ya Macho na Mtoto wa jicho kwenye Kampeni ya Upimaji Afya Bure iliyofanyika Mnazi mmoja*
Zoezi hilo linasimamiwa na Madaktari bingwa wa Macho kutoka Hospital ya Muhimbili, Hindumandal na Ebrahim Haji.
Kutokana na uhitaji kuwa mkubwa RC Makonda ameomba Taasisi hiyo kupima na kufanya matibabu kwa Wagonjwa 1,000 badala ya 500 iliyoahidi ambapo wameridhia ombi hilo.
Amesema kuwa kwa kawaida Garama za upasuaji wa Macho ni kati ya Shillingi 900,000 hadi 1,000,000 pamoja na Miwani hivyo kwa Watu 1,000 ni sawa na Kiasi cha Shilling Billion Moja lakini kupitia wadau Wagonjwa hao watapatiwa matibabu na Miwani Bure ili waone Matunda ya Serikali ya awamu ya Tano kupitia RC Makonda
RC Makonda Anawahimiza Wananchi wenye Matatizo ya Macho kufika kwenye  kambi ya matibabu ya Macho iliyopo mtaa wa Hindragand Posta kila Jumamosi na Jumapili kwa kipindi cha Miezi Miwili ili wapatiwe Vipimo, Matibabu na Miwani Bure kwa wenye uhitaji.
Ameshukuru wadau hao kwa kumuunga mkono na kueleza kuwa lengo lake ni kuwawezesha wananchi wasioweza kumudu gharama za matibabu kupata huduma.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!