Thursday 19 October 2017

Kesi ya Lulu, mdogo wa Kanumba asimulia yote.



Kesi ya mauaji inayomkabili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael (Lulu) imeendelea kusikilizwa hii leo katika Mahakama Kuu jijini Dar es salaam, kwa upande wa mshataka kuanza kutoa ushahidi wao.



Akitoa ushahidi ndugu wa marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco, ameisimulia mahakama jinsi ilivyokuwa siku ya tukio, na kwamba aligundua kuwa kaka yake hapumui baada ya kugombana na mpenzi wake Lulu.
"Siku ya tukio marehemu Kanumba alinambia nisitoke nyumbani anataka tutoke wote kuanzia saa sita usiku, akaja Lulu na Kanumba ndiye aliyemfungulia mlango Lulu, alipofika ndani nikasikia akimuuliza Lulu kwanini anaongea na boyfriend wake mbele yake? Katika malumbano yao Kanumba alikuwa akimvuta Lulu arudi ndani na Lulu naye alikuwa anataka kutoka nje, wakati wakiendelea kugombana mlango wa chumba changu sikuufunga”, alisikika Seth akiisimulia Mahakama.
Seth aliendelea kusimulia kuwa …..”Baada ya ugomvi Lulu alikuja chumbani kwangu akilia, akanambia Kanumba kadondoka amejaribu kummwagia maji haamki. Na ilikuwa mara ya kwanza kuona ugomvi kati yao, nilipoingia chumbani nilimkuta Kanumba chini kaegemea ukuta nikamlaza chali nikamtafuta daktari wake, Dk Kageiya, alipofika alimfanyia chek up akanambia ameshafariki ila akashauri tumpeleke hospitali ya Muhimbili”.
Kesi hiyo imehairishwa mpaka hapo kesho Oktoba 20, ambapo upande wa mashtaka umepanga kuja na ushahidi zaidi.
Lulu anashtakiwa kwa kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake Steven kanumba, ambaye alikuwa naye kwenye mahusiano mpaka umauti ulivyomfika April 2012.
CHANZO: EATV.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!