Thursday 12 October 2017

Kaya 1000 zakosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuteketezwa kwa moto wilayani Chunya

[​IMG]
Zaidi ya nyumba 900 zimeteketezwa kwa moto na kusababisha kaya zipatazo 1000 kukosa mahali pa kuishi baada ya kamati ya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na wakala wa huduma za misitu nchini, TFS, kuendesha zoezi la kuwaondoa watu ambao wamevunja sheria kwa kuvamia na kuishi ndani ya hifadhi ya misitu ya asili iliyopo tarafa ya Kipembawe wilayani Chunya.


Vilio na Simanzi vilisika baada ya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Chunya, Bi. Rehema Madusa kuiongoza kamati yake kuteketeza kwa moto nyumba za makazi kwa lengo la kuwaondoa wananchi ambao wamevamia hifadhi ya misitu ya asili iliyopo tarafa ya Kipembawe na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.

Grace Wille ni meneja wa wakala wa huduma za misitu, TFS, wilaya ya Chunya ambaye amesema kuwa katika tarafa ya Kipembawe kuna misitu zaidi ya saba inayohifadhiwa, lakini misitu hiyo imevamiwa na makundi ya watu ambao wanaendesha shughuli za kiuchumi na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na kwamba zoezi hilo la kuwaondoa ambalo limeanza litakuwa ni endelevu.

Baadhi ya wananchi ambao nyumba zao zimeteketezwa kwa moto wamesema wanashangazwa na hatua ya wao kuitwa wavamizi, wakati maeneo hayo huuziwa na viongozi wa vijiji huku wakidai kuwa hata baada ya kuuziwa maeneo hayo bado wamekuwa wakiendela kuchangishwa fedha na viongozi wao kwa ajili ya kuwapelekea viongozi wa juu wa serikali ili wasiondolewe katika maeneo hayo.


Chanzo: ITV

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!