Thursday, 12 October 2017

Davido ahojiwa kufuatia kifo cha rafiki yake

Davido ahojiwa kufuatia kifo cha rafiki yake
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDavido ahojiwa kufuatia kifo cha rafiki yake
Polisi katika mji wa Lagos nchini Nigeria wanasema kuwa wanamchunguzua mwanamuziki Davido, ambaye jina lake kamili ni David Adeleke, kufuatia utata unaozunguka kifo cha rafiki yake Tagbo Umeike.

Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa Davido hachukuliwa kuwa mshukiwa wakati huu, lakini akathibitisha kuwa mwanamuziki huyo wa afrobeats, aliitwa kuhojiwa pamoja na familia ya Tagbo, ambao walikuwepo wakati wa kifo chake.
Tunachunguza ni wapi Davido alienda, kanda ya video, ili kupata picha wazi kuhusu kile kilichotokea. alisema msemaji huyo.
Bw. Tagbo, rafiki yake Davido alifariki tarehe 3 Oktoba na mwili wake ukaachwa nje ya hospitali mjini Lagos.
Davido amekana kabisa kuhusika kwenye kifo cha rafiki yake.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!