Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2017. Wakimsikiliza ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na maafisa waandamizi wa Ofisi ya Rais. Picha na Ikulu
**************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Oktoba, 2017 amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kwa kuongeza idadi ya Wizara, kuteua Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya na kuwahamisha Wizara baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri.
Katika mabadiliko hayo Mhe. Rais Magufuli ameongeza idadi ya Wizara na Mawaziri wake kutoka 19 hadi 21, na Naibu Mawaziri kutoka 16 hadi 21.
Iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini imegawanywa na kutakuwa na Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini, na iliyokuwa Wizara Kilimo, Mifugo na Uvuvi imegawanywa na kutakuwa na Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mhe. Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ametangaza mabadiliko hayo Ikulu Jijini Dar es Salaam na lifuatalo ni Baraza la Mawaziri baada ya kufanyiwa mabadiliko.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Waziri – George Huruma Mkuchika
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Waziri - Selemani Said Jafo
Naibu Waziri - Joseph Sinkamba Kandege
Naibu Wazri - George Joseph Kakunda
Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Waziri - January Yusuf Makamba
Naibu Waziri - Kangi Alphaxard Lugola
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.
Waziri - Jenista Joackim Mhagama
Naibu Waziri - Anthony Peter Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira)
Naibu Waziri - Stella Alex Ikupa (Walemavu)
Wizara ya Kilimo.
Waziri - Dkt. Charles John Tizeba
Naibu Waziri - Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Waziri - Luhaga Joelson Mpina
Naibu Waziri - Abdallah Hamis Ulega
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri - Prof. Makame Mbarawa Mnyaa
Naibu Waziri - Mhandisi Atashasta Justus Nditiye
Naibu Waziri - Elias John Kwandikwa
Wizara ya Fedha na Mipango.
Waziri - Dkt. Philip Isdor Mpango
Naibu Waziri - Dkt. Ashatu Kijaji
Wizara ya Nishati.
Waziri - Dkt. Medard Matogoro Kalemani
Naibu Waziri - Subira Hamis Mgalu
Wizara ya Madini.
Waziri - Angellah Kairuki
Naibu Waziri - Stanslaus Haroon Nyongo
Wizara ya Katiba na Sheria.
Waziri - Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko
Kabudi.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri - Dkt. Augustine Philip Mahiga
Naibu Waziri - Dkt. Susan Alphonce Kolimba
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT).
Waziri - Dkt. Hussein Ali Mwinyi
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri - Mwigulu Lameck Nchemba
Naibu Waziri - Mhandisi Hamad Yusuf Masauni
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Waziri - Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla
Naibu Waziri - Josephat Ngailonga Hasunga
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri - William Vangimembe Lukuvi
Naibu Waziri - Angelina Sylivester Mabula
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri - Charles Paul Mwijage
Naibu Waziri - Mhandisi Stella Martin Manyanya
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Waziri - Prof. Joyce Lazaro Ndalichako
Naibu Waziri - William Tate Ole Nasha
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Waziri - Ummy Ally Mwalimu
Naibu Waziri - Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Waziri - Dkt. Harrison George Mwakyembe
Naibu Waziri - Juliana Daniel Shonza
Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Waziri - Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe
Naibu Waziri - Jumaa Hamidu Aweso
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Stephen Kagaigai alikuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri.
Bw. Stephen Kagaigai anachukua nafasi ya Dkt. Thomas D. Kashilila ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Wateule wote wataapisha Jumatatu tarehe 09 Oktoba, 2017 saa 3:30 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment