Friday 6 October 2017

Asilimia 12 ya vifo vyote nchini hutokana na saratani ya matiti


 Wizara ya afya katika kuadhimisha siku ya saratani ya matiti nchini imetoa elimu kuhusu saratani ya matiti na kuwahamasisha wanawake kufika vituo vya afya ili kufanya uchunguzi wa saratani hizo ili kujikinga au kupewa matibabu mapema. 

Imeelezwa kuwa saratani ya matiti ni ugonjwa wa pili Tanzania unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi zaidi wakati ugonjwa wa kwanza ukiwa ni saratni ya mlango wa kizani ambapo takwimu zinaonesha kuwa asilimia 12 ya vifo vyote nchini vinatokana na saratani ya matiti.
 Kwa mujibu wa Mratibu wa Programu ya Via vya Uzazi katika Wizara ya Afya Dr Safina Yuma ameeleza kuwa changamoto kubwa ni kwamba wanawake wengi hifika hospitali ikiwa ugonjwa wa saratani uko kwenye hatua kubwa sana na hivyo kufanya ugumu katika matibabu yake lakini pia huigharimu serikali katika kufanya kulipia matibabu hayo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!