Thursday, 5 October 2017

Ahukumiwa Jela miezi 12 kwa Kumkashifu Rais

MHASIBU wa Shule ya Sekondari ya St Joseph Cathedral, Elizabeth Asenga amehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni tano au kwenda jela miezi 12 baada ya kukutwa na hatia ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli kuwa kilaza kupitia mtandao wa ‘WhatsApp’.


Hata hivyo, mshitakiwa huyo alilipa faini na kukwepa kwenda jela miezi 12. Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alisema mahakama ilisikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kumwona mshitakiwa ana hatia. Alisema upande wa mashitaka uliita mashahidi saba, kuthibitisha mashitaka hayo dhidi ya mshitakiwa. “Mahakama inakutia hatiani kwa makosa uliyoshitakiwa nayo, hivyo utatakiwa kulipa faini ya Sh milioni tano au kutumikia kifungo cha miezi 12 jela,” alisema Hakimu Shaidi.
Kabla ya kutolewa adhabu, mshitakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu, kwa kuwa mama yake mzazi ni mzee anamtegemea na ana watoto wanaomtegemea. Katika kesi ya msingi, inadaiwa Agosti 6, mwaka jana aliwasilisha maneno kinyume cha sheria kupitia mtandao wa WhatsApp katika group la wafanyakazi la STJ kwa nia ya kumtusi Rais. Mshtakiwa alinukuliwa kuwa , “Habari za asubuhi humu hakuna rais kilaza kama huyu wetu duniani angalia anavyompa Lissu umashuhuri, fala yule picha yake ukiweka ofisini nuksi tupu ukiamka asubuhi ukikutana na picha yake kwanza siku inakuwa ya mkosi mwanzo mwisho.”

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!