Monday 2 October 2017

Afia kwa Mganga wa Kienyeji akipatiwa matibabu ya kuongeza nguvu za kiume.



Image result for tunguli
SHINYANGA: Mzee Joseph Sahn(60) afia kwa Mganga wa Kienyeji akipatiwa matibabu ya kuongeza nguvu za kiume.
- Yadaiwa Mganga huyo alikuwa akimuwekea dawa ya unga kupitia tundu la uume na kuanza kuisukuma kwa kutumia pampu ya kujazia upepo kwenye Baiskeli

Akizungumza ofisini kwake leo Jumatatu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amesema tukio hilo lilitokea jana Jumapili saa 10:00 jioni nyumbani kwa mganga huyo, alipokuwa anamuwekea dawa ya unga kupitia tundu la uume wake kisha kuanza kuisukuma kwa kutumia pampu ya kujaza upepo kwenye baiskeli.

Kamanda Haule amesema wakati akipampu ili dawa hiyo iingie vizuri ndani, mzee huyo alianza kutokwa damu nyingi kwenye tundu hilo na kisha kuishiwa nguvu. 

“Kutokana na kutokwa damu nyingi ilisababisha kifo cha mzee huyo, ambapo tayari jeshi la polisi linamshikilia mganga huyo kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mzee Joseph,” amesema Kamanda Haule

Amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili ajibu tuhuma zinazomkabili. 

Kamanda Haule aliwataka wananchi kuacha kuona waganga kuwa kimbilio la matatizo yao badala yake wakimbile hospitalini au kwenye vituo vya afya vilivyokaribu nao.


Chanzo: Mwananchi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!