Tuesday, 19 September 2017

Uwanja wa Ndege Dar kuunganisha nchi za EAC

MAMLAKA ya Usafi ri wa Anga (TCAA), imekusudia kuufanya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kuwa njia panda ya usafi ri wa anga katika eneo hili la Afrika Mashariki.


Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa anazungumzia kongamano la kwanza la wadau wa usafiri wa anga nchini linalotarajia kufanyika leo na kesho lengo likiwa ni kujadili namna ya kuinua na kuboresha zaidi sekta ya usafiri wa anga katika uchumi wa taifa.
Alisema kusudio hilo la kuufanya JNIA kuwa njia panda ni moja ya mada mbalimbali zitakazojadiliwa katika kongamano hilo, nyingine ni kuanguka ama kuporomoka kwa uchukuzi wa shehena, uhaba wa wataalamu wa usafiri wa anga, mchango wa sekta ya usafiri wa anga katika uchumi wa Tanzania na nyinginezo.
Kongamano hilo linalotarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, lenye kaulimbiu inayosema ‘Kupeleka juu Sekta ya Usafiri wa Anga,” litawashirikisha wadau zaidi ya 70 wakiwemo kampuni za ndege, vyuo vya usafiri wa anga, mamlaka ya viwanja vya ndege na wadau wengine wote wa usafiri wa anga.
“Kongamano hili ambalo ni la kwanza la aina hii kufanyika nchini limedhamiria kukutanisha wadau wote muhimu wa usafiri wa anga ili kujadili mafanikio, changamoto na kupanga mikakati ya kukuza sekta ya usafiri wa anga ili itoe mchango stahiki katika kukuza uchumi wa nchi na hivyo kufikia azma ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025,” alisema.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!