Monday, 11 September 2017

TAASISI YA NIMR YABAINI SABABU NA VYANZO VYA VIFO KATIKA HOSPITALI NCHINI TANZANIA BH

Na Binagi Media Group
Utafiti mpya uliofanywa na Taasisi ya Taifa Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini (NIMR) umebaini kwamba magonjwa ya Malaria, Ukimwi, Moyo, Mfumo wa Upumuaji pamoja na Upungufu wa Damu yanayongoza kwa kusababisha vifo vya hospitalini.


Aidha utafiti huo ambao uliofanyika mwaka jana kwa kutumia takwimu za kuanzia mwaka 2006 hadi 2015 katika hospitali 39 nchini ambazo ni pamoja na hospitali ya Taifa, hospitali za Kanda, Hospitali za mikoa na wilaya umeonyesha kwamba vifo vya ajali vimeongezeka kwa asilimia 16, saratani asilimia 24, kiharusi asilimia 27 na kisukari asilimia 11.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza hii leo Jijini Mwanza kwenye uwasilishaji wa matokeo ya utafiti huo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na Kanda ya Magharibi, Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subi amesema hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa kwa kutumia utafiti huo ili kudhibiti vifo hivyo.

Mtafiti Mkuu Kiongozi kutoka NIMR, Dkt.Leonard Mboera amesema utafiti huo pia ulilenga kuangalia upatikanaji wa takwimu za vifo katika hospitali nchini Tanzania ambapo ilibainika kuwepo changamoto katika ukusanyaji, uchanganuzi na matumizi ya takwimu katika hospitali.

Taasisi ya NIMR ilifanya utafiti ili kubaini sababu na vyanzo vya vifo katika hospitali nchini Tanzania na kubaini kwamba ugonjwa wa Malaria unaongoza kwa kusababisha vifo kwa asilimia 12.8, Mfumo wa upumuaji kwa asilimia 10.1, Ukimwi asilimia 8.0, upungufu wa damu asilimia 7.8, magonjwa ya moyo na mfumo wa damu asilimia 6.3 huku mikoa ya Dar es salaam, Mwanza na Morogoro ikiongoza kwa vifo katika hospitali nchini.

Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi akizungumza kwenye warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella. Warsha hiyo imejumuisha washiriki kutoka mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita, Tabora, Shinyanga, Mara, Simiyu na Mwanza.
Dkt.Changalucha John ambaye ni Mkurugenzi Mkuu NIMR kituo cha Mwanza akizungumza kwenye warsha hiyo
Mtafiti Mkuu Kiongozi kutoka NIMR, Dkt.Leonard Mboera, akizumza na wanahabari nje ya warsha hiyo
Dkt.Omari Gamuya akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Mganga Mkuu mkoani Mara
Mmoja wa watafiti kutoka NIMR akifafanua jambo mbele ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuhusu utafiti huo
Washiriki wa warsha hiyo
Baadhi ya washiriki
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Leonard Subi (wa tatu waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na washiriki mbalimbali wa warsha hiyo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!