Taarifa zilizotufikia kutoka Nairobi Kenya kuhusiana na hali ya mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu kuhusu hali yake baada ya kufanyiwa upasuaji ni kuwa ametolewa katika chumba cha upasuaji na sasa yupo ICU kwa uangalizi.
Mh Tundu Lissu ametolewa salama katika chumba cha upasuaji baada ya Masaa 7 tangu saa nne asubuhi hadi sasa saa kumi na Moja jioni na upasuaji umefanyika kwa mafanikio hivyo yupo Executive ICU kwa uangalizi wa karibu zaidi
Tutaendelea kuwajuza. Na tunawahakikishia kuwa madaktari wametueleza hakuna tishio lolote kiafya yuko macho na fahamu zote na hii ndio ilikuwa hatua ngumu na Mungu ametupitisha hivyo tuendelee kumuombea apone haraka
Hemedi Ali
Mkuu wa idara ya Uenezi CHADEMA.
Nairobi hospital.
Mkuu wa idara ya Uenezi CHADEMA.
Nairobi hospital.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mchana wa September 7 2017 nyumbani kwake ndani ya gari Area D Dodoma, baada ya kurudi akitokea Bungeni kupata chakula cha mchana, hivyo amepelekwa Nairobi kwa matibabu.
KWA HISANI YA MILLARDAYO:COM
No comments:
Post a Comment