Thursday 7 September 2017

Rais Magufuli apokea ripoti za Bunge kuhusu Almasi na Tanzanite, awataka wateule wote waliotajwa wakae pembeni

Image may contain: 1 person, standing and suit
IKULU: Rais Magufuli mara baada ya kupokea ripoti za Tume za Bunge kuhusu biashara ya Almasi na Tanzanite amsema wateule waliotajwa kwenye ripoti wanatakiwa wakae pembeni. Hawawezi kuchunguzwa wakiwa wapo Serikalini.


- ⁠⁠⁠⁠⁠Rais pia amesema kuwa Serikali ilikusanya taarifa za kutosha kutoka kwenye kompyuta za wawekezaji wa madini.


Mh Dotto, mwenyekiti wa kamati ya Tanzanite
=>Mh rais nimshukuru pia mh spika kwani hakutuingilia katika mchakato wa kufanya kazi hii.

=>Niwashukuru pia wajumbe wa kamati yangu

=>Tulipitia Jumla nyaraka 150 kutoka taasisi za serikali na taasisi binafsi.

=>Mkataba wa STAMICO wa almasi ni wa kinyonyaji na hauna tija kwa nchi. Tumependeza mkataba huo uvunjwe.

=>Ajira zinazotokana na tanzanite India ni zaidi ya watu 500,000

=>Tunaomba mfumo wa udhibiti wa madini ya Tanzania uangaliwe upya

=>Tuwe na sheria maalumu inayosimamia mfumo na udhibit wa uchimbaji wa madini haya haya.

=>Tuliangalia mkanda wa video unaoonyesha wizi wa madini ya Tanzania wakishirikiana na watanzania.

=>Mh rais umeamua kuonyesha mfano wa kusonga mbele na kutogeuka jiwe.

=>Mh rais nashukuru kwa kibali chako naomba nikomee hapa.
Mh waziri mkuu wa JMT, Kasim Majaliwa Majaliwa

=>Kamati hizi mbili zimefanya kazi kubwa na kamati hizi zimetokana jitihada zako mh rais.

=>Mimi ningeweza kushughulikia na kuwaita mawaziri na kumpangia kila mtu majukumu yake

=>Kwa kuwa mh rais umeamua suala hili liwe la kizalendo na wazi kwa kila mtanzania na ndiyo maana nikaamua kukuletea ulishughulikie suala hili.

=>Kwa niaba yako na niaba ya serikali, natumia nafasi hii kumshukuru spika na wabunge kwa namna walivolishughulikia suala hili.

=>Ndugu watanznai, Tanzania ni yetu, lazima tushikamane pamoja tuijenge nchi yetu. Lazima tushikamane ili rasilimali zetu zitunufaishe watanzania.

=>Kamati imeonyesha udhaifu mkubwa wa usimamizi wa madini.

=>Watanzania wale waliona hawahudumiwi, sasa lazima waone wanahudumiwa.

=>Mh rais tunajua unazo njia nyingi sana za kupata taarifa. Na sisi ndio njia mojawapo ya kukusaidia kupata taarifa. Sina mashaka na wewe kwamba taarifa hii itakupa faraja.

=>Nisingependa kuongea mengi maana wananchi wana hamu ya kuona ripoti hii inakabidhiwa na hatua stahiki zinachukuliwa.

=>Mh rais sasa nipo tayari kukukabidhi ripoti hii ya kamati ili kuweza kuona hatua stahiki zinachukuliwa.

Kamati ya almasi imeanza kukabidhiwa, ikifuatiwa na kamati ya Tanzanite

Rais wa JMT Mh John Pombe Magufuli anaanza kuhutubia.

=>Noamba kumshukuru Mh spika pamoja na kamati hizi mbili kwa kazi kubwa ya kuchunguza madini ya almasi na Tanzanite.

=>Taarifa hii inakumbusha hali halisi kwa jinsi taifa letu limekuwa likichezewa.

=>Wakati napokea taarifa ya kwanza na ya pili, nilikuomba mh spika bunge likasaidie kwenye upande wa almas na tanzanite.

=>Na siku moja ulinipigia simu ukaniambia unaenda kuunda hii kamati na ulikuwa hujua utaenda kuwateua akina nani.

=>Nchi yetu imechezewa sana, na hao wanaotuchezea sijui kama wanajua kama sisi ni binadamu au ni kitu gani.

=>Ukitembelea mgodi wa almasi au Tanzanite, utaona maosha ya wananchi walioko pale, angalia maisha halisi ya wananchi wa tanznaia.

=>Tanzania hata ni nchi ya pili duniani kwa vivutio duniani.

=>Mh Zungu ameongelea kiasi cha madini yaliyoko pale.

=>Wakati tunaanza kufanya research ya mambo haya. Baadhi ya watu walifikiri tunaongea kutoka hewani.

=>Tuna data zao zote, email zao zote. Wamekuja kushtuka wakabadilisha kompyuta na ilikuwa too late.

=>Ndiyo maana hawa wazungu wanaofanya mazungumzo ya dhahabu walianza 14 sasa wameongezeka hadi 25. Wanaenda wanarudi lakini sisi watu wetu ni walewale.

=>Uhuru wa kweli ni uchumi, ambao utalisha watoto wako, utaendesha shule, utatengeneza barabara.

=>Hili suala la Tanzanite na mh waziri mkuu nafikiri mtanikabidhi flashi. Mimi nilikuwa na flash yangu kabla(Mh rais anatoa flash kwenye koti lake na kuionesha).

=>Kunapokuwa na vita, lazima na baadhi ya watu wanapelekwa upande wa maadui.

=>Napenda kuwaambia katika vita hii wapo

=>Thamani iliyokuwa inazungumza kwamba ni dola milioni 14 inawezekana ni dola M 20 au zaidi ya hapo.

=>Wizara ya madini haina vifaa vya kupimia madini hata beam balance.

=>Sasa niwaambie anayefanya hiyo kazi na maadui ni Profesa Mruma na aliyetuletea data ni Profesa Mruma.

>Napenda kuwahakikishia, yote yaliyoandikwa humu nitayashughulikia.

=>Ripoti hii itanisaidia kujua hata jinsi ya kuwachagua wasaidizi wangu.

=>Kama ulivosema ripoti wengi waliotajwa ni wanasiasa hasa wabunge. Najua mna kamati ya bunge ambayo mtaweza kuwashughulikia huko. Pia kuhusu kuandika barua kwenye chama.

=>Kuna wateule waliotajwatajwa wengine nimewateua mwenyewe, na wengine wanaonekana wachapakazi. Kwasababu mimi ndiye niliowateua. Kwasababu hizi ripoti nimezipokea mimi.

=> Kwanza naagiza vyombo vya ulinzi na usalama vifuatilie haraka
=>Wale wote waliotajwa ambao wametajwa, ili vyombo vya usalama vifanye kazi vizuri ni matumaini yangu mtakaa pembeni.

=>Nayazungumaza haya siyo kwasababu nawachukia watu, lakini tunaibiwa mno.

=>Unavyosaini mkataba mkubwa namna hiyo

=>Inawezekana tatizo ni mfumo kama mlivyosema kwenye ripoti yenu, lakini kama tatizo ni mfumo basi fumuka.

=>Nilisikia wengine wanatishia eti wanapunguza wafanyakazi. Nilitamani waseme wameondoka kabisa! Tungewapa wananchi wachimbe ili watengeneze ajira.

=>Kama Tanzanite inatoka eneo moja tuu Tanzania, BOT walishindwa kuweka kituo kimoja cha kununua tanzanite na kutengeneza reserve? Nani aliyetuloga?

=>Mh spika na waheshimiwa wabunge napenda kuwashukuru sana.

=>Riport hii ingekuwa ni ya juujuu ningeunda tume ya wataalam ichunguze na kulinganisha matokeo.

=>Sisi tutaifanyia kazi na naomba ofisi ya waziri mkuu ikutane na wataalam wa idara zinazohusika na ofisi ya mwanasheria mkuu.

=>Kwa mfano wabunge wangepewa tanzanite kila mtu mbilimbili wasingeonesha madudu haya.

=>Kwasasa uchumi wetu unakuwa kwa 7% na ni wanne. Hii tanzanite ingekuwa inatumika inavyopaswa tungekuwa mbali.

=>Maslahi ya vyama vyetu tuyaweke pembeni, tuyaweke maslahi ya nchi mbele.

=>Ni mara kumi uvunje sheria lakini ulinde fedha za watanzania.

=>Nipende kuwashukuru wote mliojitoa kwa ajili ya kulinda rasilimali zetu.

=>Naomba niwakabidhi vyombo vya ulinzi na usalama

=>Nimeamua kuwakabidhi ripoti ili wakaanze kufanya kazi. Tumeibiwa mno.

=>Ni bora wakuchukie, uonekane siyo mwanasiasa mzuri kwasababu ni hukuja kutafuta mchumba.

=>Ninawaomba ndugu zangu tushirikiane katika hili. Nchi yetu imechezewa mno mno.

=>Niwashukuru wote, Mungu awabariki wote, Mungu ibariki Tanzania

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!