Tuesday, 12 September 2017

Rais Magufuli amtembelea Meja Jenerali Mstaafu, Vincent Maritaba aliyelazwa Hospitali ya Lugalo baada ya kushambuliwa kwa risasi jana.

[​IMG]

Meja Jenerali mstaafu wa JWTZ, Vincent Mritaba amepigwa risasi 5 na watu wasiojulikana akiwa anaingia nyumbani kwake, Tegeta Dar es Salaam ambapo watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamemshambulia kwa risasi Meja Jenerali huyo

Tukio hilo limetokea jana jioni wakati Meja Jenerali Mritaba akiingia Nyumbani kwake Tegeta ambapo alivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa risasi. 

Hadi usiku wa jana Madaktari walikua wanaendelea na upasuaji kutoa risasi tatu tumboni na kushughulikia majeraha mengine katika hospital ya Lugalo.
[​IMG]
[​IMG]

[​IMG]

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!