Saturday 9 September 2017
DON WILLIAMS AFARIKI DUNIA
Donald Ray Williams enzi za uhai wake..
MKALI wa muziki wa country, Donald Ray Williams ‘Don Williams’, amefariki dunia.
Williams alifariki jana Ijumaa akiwa nyumbani kwake Alabama, nchini Marekani.Williams aliyekuwa maarufu duniani kote kwa muziki wa country, alitamba na vibao kadhaa kikiwamo kile cha ‘I Believe in you’ alichokitoa mwaka 1981, amefariki dunia akiwa na miaka 78 baada ya kuugua kwa muda mfupi.Mbali na ‘I Believe in you’, vibao vingine maarufu vya Williams ni pamoja na Some Broken hearts never mend, Love me tonight, Lay down beside me na vinginevyo.Pamoja na umaarufu wake katika muziki, Williams hakuwa mtu mwenye makuu na aliyapenda maisha ya kawaida kiasi cha kubatizwa jina la “the Gentle Giant”.Williams aliyezaliwa mwaka 1939, alianza kupenda muziki akiwa Portland kabla ya kuhamia Nashville miaka ya 1960 ambako umaarufu wake ulitapakaa duniani kote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment