Wednesday 13 September 2017

DAR: Jeshi la Polisi limeripoti kumuua anayedaiwa kuwa kinara wa ujambazi katika mabenki, Rashid Kapela aliyeongoza mauaji ya askari nane huko Kibiti.

Image may contain: 1 person, smiling
Jeshi la Polisi limeripoti kumuua anayedaiwa kuwa kinara wa ujambazi katika mabenki, Rashid Kapela aliyeongoza mauaji ya askari nane huko Kibiti.


- Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, amesema kuwa Jambazi huyo amewataja baadhi ya wahalifu wakuu anaotenda nao uhalifu huo.
Kamanda Mambosasa leo hii ameongea na waandishi wa habari na kutoa taarifa kwa umma. Amezugumzia hali ya uhalifu na kesi mbalimbali nchini

Kamanda Mambosasa anaongea:
Kikosi cha Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam kupitia kikosi cha maalum cha kupambana na majambazi, mnamo Sept 12, 2017 majira ya saa nne usiku huko maeneo ya Kivule - Chanika tulimuua Jambazi Sugu aliyeshiriki matukio mbalimbali. jambazi huyo alikuwa naitwa Anae Rashid Kapela maafuru kwa jila la Abuu Mariam

Tulipiga ambush kwenye nyumba aliyokuwemo, tulipojaribu kumsimamisha akaanza kukimbia. Akapigwa risasi kwenye goti akaanguka. Alipokamatwa alitaja mlolongo wa matukio aliyoshiriki.

Jambazi huyo alikiri kushiriki kwenye matukio ya kuuwawa kwa askari polisi pale Mbande, NMB Mkuranga, Access Bank Mbagala, Alishiriki pia kwenye matukio ya Kibiti na kuua askari 8, pamoja na kuchukua silaha. Yeye ndiye alikuwa kiongozi wa kundi.

Amewataja baadhi ya wahalifu wakuu anaotenda nao uhalifu huo.

Askari walimkimbiza kumpeleka Muhimbili lakini alifia njiani baada ya kutokwa damu nyingi.

Baada ya kumpekua alikutwa akiwa ana majeraha matatu ya risasi, tofauti na niliyoyaelezea. Lakini pia tulimkuta na kidonda, kibichi kabisa ambavyo vilimfanya aende kutibiwa kwa bibi mmoja (majeraha matatu).

Tukio la pili: Kupatikana kwa Silaha 3 (short gun) na bastola 2 na risasi 30
Mnamo september 8 2017 majira ya saa tano usiku maeneo ya Gezaulole: Jambazi mmoja alikamatwa akiwa na bastola moja aina ya noringo (00539 namba za usajili) ikiwa na risasi 14 ndani ya magazine. Alikuwa na mwenzie mmoja aliyeenda kwenye duka la mfanyabishara aliyefahamika kwa majina ya Ramadhani Ismail (22) wakitaka kufanya uporaji. Walifanikiwa kupora Tshs. 500,000 na simu 2 za wateja.

Wakati jambazi huyo anaondoka, raia mmoja alifanikiwa kumtupia jiwe la mzani likampiga na kumwangusha.

Wananchi walifanikiwa kumnyang'anya silaha yake na kumshambulia na kumuua!

Jambazi huyu pia kabla ya kufa kwake alikiri kushiriki wizi wa pikipiki na bajaj kadhaa. Ni mwizi sugu ambaye alikuwa akifuatiliwa kwa muda mrefu.

Kanda maalum imepiga marufuku uuzwaji wa silaha za jadi hadharani. Mapanga, visu na manati! Maeneo sugu kwa uuzaji ni Ubungo na maeneo kiasi ya TAZARA. Tutawasaka wanaofanya biashara hizo.

Kuvunjwa kwa ofisi ya Mawakili:
Sept 12 majira ya saa 7 na dk 45 usiku taarifa ilitolewa kuhusu tukio hili. Safe ya nyaraka mbalimbali ikiwa na pesa viliporwa na wezi. Ni wakili wa kujitegemea na Manji ni mmoja wa wateja wa ofisi yao.

Mpaka sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kosa hili.

Tukio la Meja Jenerali Mstaafu, Vicent Kariongo kushambuliwa (Tegeta Masaiti):

Mhusika alikuwa ameenda Benki pale Mbezi Tangi Bovu; baada ya kufanya muamala vijana wawili wakiwa na pikipiki walimfuatilia. Alipofika getini alipiga honi na nyumba yake inalindwa na askari wa Suma JKT.

Askari alifanya kosa kwa kufungua mlango na wahalifu wakafanya shambulizi. Aliamriwa na waarifu akimbie akakimbia akaacha silaha yake! Na huyu ana mafunzo ya JKT. Lilikuwa ni kosa kufungua geti bila kuwa na silaha. Hakupigwa hata kofi na waarifu! Tunaendelea kumshikilia.

Eneo la tukio tulipofika tumebaini kulikuwa na mtu aliyekuwa anafanya mawasiliano kati ya mtoa huduma na mpokea huduma (NBC Tangi Bovu).

Magunia 12 ya Bangi na lita 21 za Gongo:
Tumewatia mbaroni washtakiwa 3 mmoja akiwa na Prado mpya na yenye hali nzuri kabisa ambayo huwezi kuitilia mashaka kuwa inaweza kubeba mzigo huu. Wahusika walipokamatwa, gari hilo lilikuwa limebeba mzigo huo. Tutaiomba mahakama kutaifisha gari hilo.

Vita dhidi ya madawa ya kulevya ni ya kudumu! Wanaoshiriki hawatabaki salama.

Kampeni ya Ukamataji wa Makosa yanayohusiana na Usalama Barabarani:

Tangu Sept 09 hadi Sept 11 tumeendesha oparesheni na kukamata magari 13,220 na pikipiki 256. Kuna waliokubali makosa wakalipa faini; zilipatikana Sh. 475,350,000 na ni kiwango kikubwa. Watu hawajawa tayari kutii sheria za usalama barabarani.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!